Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, June 12, 2013

KENYA NA MALAWI ZATOKA SARE YA 2-2

Late own goal sees Malawi heldTimu za Taifa za Malawi na Kenya zimetoka sare kwa kufungana mabao 2-2 mjini Blantyre katika  mechi ya kufuzu kombe la dunia.

Malawi ndio walikuwa wanaongoza kwa mabao 2-1 lakini katika dakika ya mwisho Chimango Kayira alijifunga na kupunguza  uwezekano wa Malawi kusonga hatua inayofuata.

The Flames ndio waliowa kuwa wa kwanza kupata  bao katika  dakika ya 46, bao lililofungwa na Robion Ngalande, lakini dakika sita baadaye Mohamed Jamal akaisawazishia Harambee Stars.

Katika dakika ya 81, Robert Ng'ambi alifunga bao la pili kwa Malawi, kabla ya Kayira kujifunga na mechi kumalizikia mabao mawili kwa mawili.Matokeo hayo yana maana kwamba mabingwa wa Afrika Nigeria ndio watakaofuzu hatua inayofuata kutoka kundi F, ikiwa wataishinda Namibia mjini Windhoek, mechi inayochezwa baadaye usiku huu.

Hadi kufika leo kumebakia mwaka mmoja, kabla ya fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 kuanza nchini Brazil.

No comments:

Post a Comment