Redd's Miss Tanzania 2012 Brigitte
Alfred, alitua jana mjini Bukoba na leo tarehe 13 Desemba 2012
ametembelea Shule maalum ya Mugeza Mseto, inayofundisha wanafunzi wenye
ulemavu, pia ametembelea Kituo cha Nusura ambacho kinatunza watoto
yatima kilichopo eneo la Kashai.
Mrembo Brigitte Alfred, ambaye pia
ni Balozi wa Walemavu wa ngozi, [Albinos] ametoa misaada ya kijamii
katika vituo hivyo. Vifaa hivyo ni pamoja na Fimbo maalum za kutembelea
walemavu wasioona, Miwani, Kofia na Madawa ya ngozi kwa ajili ya
Walemavu wa ngozi. Pamoja na vyakula.
Redds Miss Tanzania 2012 pia
atatembelea Wilaya ya Misenyi Kesho na kutoa misaada kama hiyo katika
kituo kimoja kilichopo wilayani hapa.
Ziara ya Miss Tanzania 2012 imedhaminiwa na Optima Lodge & Safaris pamoja na Victoria Perch Hotel zote za Mkoani Kagera.
Kabla ya kurejea jijini DSM Redds Miss Tanzania 2012 ataelekea Mwanza kwa shughuli zingine za kijamii
No comments:
Post a Comment