Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, December 19, 2012

MBWANA SAMATTA,THOMAS ULIMWENGU NA JOHN BOCCO KUIKOSA ZAMBIA


NYOTA watatu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars,' wanatarajia kukosa mchezo wa kirafiki wa Kimataifa dhidi ya Zambia, utakaochezwa siku ya jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wachezaji hao ni washambuliaji John Bocco, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaochezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya DR Congo, ambao ni wagonjwa.
Akizungumza leo Daktari wa timu hiyo, Mwanandi Mwankemwa alisema Bocco hataweza kucheza kutokana na kuumia goti katika michuano ya Kombe la Chalenji iliyomalizika Desemba 8, mwaka huu Kampala Uganda.
Mwankemwa alisema, pamoja na kukosa mchezo huo, ataendelea kuwepo kambini kwani aliumia akiwa kwenye timu hiyo.
Akifafanua kuhusu Samatta na Ulimwengu, alisema wao waliumia wakiwa na timu yao ya TP Mazembe na wamekuja na vyeti vinavyoonyesha kuwa wagonjwa.
Mwankemwa alisema, cheti cha Ulimwengu kinaonyesha aliumia goti la mguu wa kulia na Samatta yeye kinaonyesha aliumia bega.
Wachezaji hao ambao waliwasili nchini na kuendelea kukaa nyumbani, juzi walipelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufanyiwa kipimo cha MRI ili wapate tiba sahihi.
Alisema wanasubiri vipimo vya daktari kutoka Muhimbili ila  kweli wachezaji hao ni majeruhi na wataendelea kuwatibu ili waweze kupona.
"Tunawatibu ili tutakapoingia kambini Januari 6, mwakani kujiandaa na  mashindano ya Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON), wawe wamepona kabisa', alisema Mwankemwa.
Wapinzani wa Stars walitua leo jioni nchini kwa ajili ya mchezo huo, ambao utachezwa kuanzia saa 10 kwenye uwanja wa Taifa.

No comments:

Post a Comment