LIGI KUU TANZANIA BARA 2012/2013
Michuano ya Ligi Kuu kuwania ubingwa
wa Tanzania Bara kwa msimu wa 2012/2013 itaanza Septemba 15 mwaka huu kwa timu
zote 14 kujitupa kwenye viwanja tofauti.
Mechi za ufunguzi zitakuwa kati ya
Simba vs African Lyon (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam), Polisi Morogoro vs
Mtibwa Sugar (Jamhuri, Morogoro), Tanzania Prisons vs Yanga (Sokoine, Mbeya),
Mgambo JKT vs Coastal Union (Mkwakwani, Tanga), JKT Ruvu vs Ruvu Shooting (Azam
Complex, Dar es Salaam), Kagera Sugar vs Azam (Kaitaba, Bukoba) na Toto
Africans vs Oljoro JKT (Kirumba, Mwanza).
Mzunguko wa kwanza (first round)
utamalizika Novemba 11 mwaka huu ambapo kwenye mzunguko huo mechi ya watani wa
jadi Yanga na Simba itachezwa Oktoba 3 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Ligi hiyo itamalizika Mei 18 mwakani
kwa mechi kati ya Toto Africans vs Ruvu Shooting (Kirumba), Mgambo JKT vs
African Lyon (Mkwakwani), JKT Ruvu vs Mtibwa Sugar (Azam Complex), Tanzania
Prisons vs Kagera Sugar (Sokoine), Simba vs Yanga (Uwanja wa Taifa), Oljoro JKT
vs Azam (Sheikh Amri Abeid Kaluta) na Polisi Morogoro vs Coastal Union
(Jamhuri).
Endapo Simba na Azam hazitafanikiwa
kuvuka hatua mojawapo ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la
Shirikisho, ratiba hiyo itafanyiwa marekebisho.
No comments:
Post a Comment