MPOGOLO: Usafi ni jukumu la jamii yote, aonya watu wachafu, hawana nafasi DSM
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amesisitiza kuwa usafi wa mazingira si jukumu la mtu mmoja, bali ni wajibu wa kila mwananchi, akiwataka wakazi wa Dar es Salaam kushiriki kikamilifu katika kulinda na kutunza mazingira ya Jiji.
Mpogolo ametoa msisitizo huo leo Oktoba 17,2026 mara baada ya kuhitimisha zoezi usafi eneo la minazi mirefu mtaa wa Kivukoni, akisisitiza kwamba usafi ni agizo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, la kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama
Amesisitiza kuwa Serikali haitavumilia tabia za baadhi ya watu wanaotupa taka ovyo, kuchafua maeneo ya umma na kukwamisha juhudi za usafi, akionya kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote watakaobainika kukiuka taratibu za utunzaji wa mazingira.
Aidha, Mpogolo amewataka wananchi kubadili mtazamo na kuachana na tabia ya kusubiri mamlaka pekee kufanya usafi, akibainisha kuwa kila mtu ana wajibu wa kuhakikisha eneo analoishi, kufanyia biashara au kupita linakuwa safi.

Post a Comment