Mkeka wa aina yake,Rais Samia Afanya Uteuzi, Ahamisha
Katika kuboresha utendaji kazi wa Serikali na kutokana na baadhi ya viongozi kustaafu kazi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi na uhamisho mkubwa wa Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya, na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu jijini Dodoma tarehe 29 Septemba, 2026, na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Bakari S. Machumu, maamuzi haya yameanza kutekelezwa mara moja
Uteuzi huo umewahusisha viongozi mbalimbali wakiwemo Bw. Festo Kiswaga aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Bi. Neema Lugangira aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Bw. Vita Rashid Kawawa aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang', na Bw. Richard Atufigwege Kasesera aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero
Aidha, kufuatia taarifa hiyo ya awali, Ikulu ilitoa ufafanuzi na nyongeza inayohusu mabadiliko ya baadhi ya Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri ili kuweka mambo sawa
Mabadiliko haya yote kwa ujumla yanalenga kuimarisha uwajibikaji, kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya wananchi, na kuhakikisha taasisi za serikali za mitaa zinakuwa na viongozi thabiti wanaosimamia maono ya Serikali ya Awamu ya Sita
A. Uteuzi na Uhamisho wa Wakuu wa Wilaya
Uteuzi:
Bw. Nicodemus Tambo Mwikozi ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.
Bw. Maiko Richard Kachoma ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato.
Bw. Edwin Mathew ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga.
Bi. Zaytun Seif Swai ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe.
Bw. Atupele Frank Mwakibete ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilolo.
Bw. Mtella Allam Mwampamba ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Uvinza.
Bw. Musa Ramadhani Sima ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Newala.
Bi. Sozi George Ngate ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chunya.
Bw. Mbwana Rajabu Kambangwa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya Mbulu.
SACP Selemani Enock Nyakulinga ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibondo.
Luteni Kanali Robert Augustino Kakomangile ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro.
Luteni Kanali Fortunatus Beda Kipeta ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibiti.
Luteni Kanali Joseph Athanas Murimi ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kasulu.
Bw. Festo Kiswaga ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe.
Bi. Neema Lugangira ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.
Bw. Vita Rashid Kawawa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang'.
Bw. Richard Atufigwege Kasesera ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero.
Dkt. Francis Daudi Mlacha ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama.
Bw. Mwita Petro Marwa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi.
Bw. Stanslaus Shing'oma Mabula ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rorya.
Bw. Christopher Andendekisye Kitwika ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Uyui.
Bi. Mwanaidi Adadi Rajabu ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Pangani.
Uhamisho wa Wakuu wa Wilaya:
Mhe. Grace Henry Kingalame amehamishwa kutoka Wilaya ya Nyang'wale kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Meatu.
Mhe. Fauzia Hamidu Ngatumbura amehamishwa kutoka Wilaya ya Meatu kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi.
Mhe. Hashim Shaibu Mgandilwa amehamishwa kutoka Wilaya ya Kilindi kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Babati.
Mhe. Almishi Issa Hazali amehamishwa kutoka Wilaya ya Hanang' kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa.
Mhe. Mayeka Simon Mayeka amehamishwa kutoka Wilaya ya Kongwa kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo.
Mhe. Dkt. Khamis Athumani Mkanachi amehamishwa kutoka Wilaya ya Urambo kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyang'wale.
Mhe. Kanali Isack Anton Mwakisu amehamishwa kutoka Wilaya ya Kasulu kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Misenyi.
Mhe. Michael John Semindu amehamishwa kutoka Wilaya ya Mbulu kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Sikonge.
Mhe. Mwinyi Ahmed Mwinyi amehamishwa kutoka Wilaya ya Arumeru kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga.
Mhe. Peter Ambrose Lijualikali amehamishwa kutoka Wilaya ya Nkasi kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo.
Mhe. Nickson Simon John amehamishwa kutoka Wilaya ya Kibaha kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Songwe.
Mhe. Fadhil Emmanuel Nkurlu amehamishwa kutoka Wilaya ya Songwe kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha.
Mhe. Halima Habib Okash amehamishwa kutoka Wilaya ya Chemba kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mafia.
Mhe. Rukia Ally Zuberi amehamishwa kutoka Wilaya ya Mwanga kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai.
Mhe. Hassan Omary Bomboko amehamishwa kutoka Wilaya ya Hai kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mwanga.
Mhe. Dkt. Khalfan Boniface Haule amehamishwa kutoka Wilaya ya Rorya kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda.
Mhe. Maulid Hassan Dotto amehamishwa kutoka Wilaya ya Mvomero kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Malinyi.
Mhe. Amina Nassoro Makilagi amehamishwa kutoka Wilaya ya Nyamagana kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magu.
Mhe. Jubilate Win Lauwo amehamishwa kutoka Wilaya ya Magu kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana.
Mhe. Aziza Ally Mangosongo amehamishwa kutoka Wilaya ya Mafia kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chemba.
Mhe. Wilman Kapenjama Ndile amehamishwa kutoka Wilaya ya Songea kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ileje.
Mhe. Ngolo Ng'waniduhu Malenya amehamishwa kutoka Wilaya ya Namtumbo kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Songea.
Mhe. Frank John Nkinda amehamishwa kutoka Wilaya ya Kahama kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkalama.
Mhe. Hamad Rajab Mbega amehamishwa kutoka Wilaya ya Mbozi kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo.
Mhe. Farida Salum Mgomi amehamishwa kutoka Wilaya ya Ileje kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi.
Mhe. Mohamed Mussa Mtulyakwaku amehamishwa kutoka Wilaya ya Uyui kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nkasi.
B. Uteuzi na Uhamisho wa Makatibu Tawala wa Wilaya
Uteuzi:
Bw. Ali Said Ali ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke.
Bw. Imani Lunogelo Fute ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kongwa.
Bi. Mwanaid Ramadhani Nondo ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea.
Bi. Jane Daniel Mallongo ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyan'gwale.
Bi. Leah Mbeke ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Hanang'.
Bw. Shabani Ferdinand Manyama ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda.
Bw. Mjata Daffa Abdallah ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Bahi.
Bi. Florida Julius Lulandala ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Moshi.
Bw. Shaaban Mursadi Mtengeti ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbozi.
Bw. Juma Nyasa Juma ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Rufiji.
Bw. Jafari Abdallah Kikoti ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Korogwe.
Bw. Alexander Alfonce Mhando ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Singida.
Uhamisho wa Makatibu Tawala wa Wilaya:
Bi. Mwanamvua Bakari Muyombo amehamishwa kutoka Wilaya ya Bahi kwenda kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Simanjiro.
Bi. Upendo Marango amehamishwa kutoka Wilaya ya Kibondo kwenda kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Masasi.
Bi. Fatima Said Kubenea amehamishwa kutoka Wilaya ya Masasi kwenda kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kibondo.
Bw. Athumani Saidi Likeyekeye amehamishwa kutoka Wilaya ya Hanang' kwenda kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Newala.
C. Uteuzi na Uhamisho wa Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri
Uteuzi:
Bw. Elikana Daud Zabron ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.
Bw. Agape Peter Fue ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema.
Bw. Samson Abas Sanga ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
Bi. Warda Abeid Maulid ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha.
Bw. Charles Ambokile Mwaitege ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama.
Bw. Winfrid Erneus Tamba ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido.
Bi. Dinah Edward Msuya ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.
Bi. Anna Lazaro Urio ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga.
Bw. Rashid Juma Muhaya ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo.
Bw. Felix Joseph Tinkasimile ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi.
Bw. Niceforus Martin Mgaya ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.
Bw. Idrisa Musa Naumanga ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa.
Bw. Dadi Horace Kolimba ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Bw. William Mathew Makufwe ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe.
Bw. Shaban Juma Mchomvu ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi.
Bw. Ramadhani Ali Kimara ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti.
Bi. Naima Bakari Chondo ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza.
Uhamisho wa Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri:
Bi. Fatima Hussein Laay amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.
Bw. Anderson David Msumba amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mtama kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba. (Angalia ufafanuzi zaidi chini)
Bw. James Michael John amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.
Bi. Ikupa Mwasyoge amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo.
Bw. Philimon Mwita Magesa amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Tanga.
Mhandisi Juma Hamsini Seph amehamishwa kutoka Halmashauri ya Jiji la Tanga kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma.
Bw. Kisena Magena Mabuba amehamishwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.
Bi. Beatrice Claver Mwinuka amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo.
Bi. Happiness Joachim Msanga amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe.
Bi. Upendo Eric Mangali amehamishwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.
Bw. Jamal Idrisa Abdul amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni.
Bw. Diocles Mugishagwe Rutema amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya Kibondo kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima.
Bw. Binuru Mussa Shekidele amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha.
Bw. Sunday Ndori Deogratius amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'wale.
Bi. Husna Toni Chambo amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'wale kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala.
Bw. Duncan Golden Thebas amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Newala kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mwanga.
Bw. Mashaka Said Mfaume amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe.
Bw. Majid Hemed Mwanga amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mlele kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.
Bi. Hellen Mwambeta amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Siha kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Bi. Rehema Said Bwasi amehamishwa kutoka Halmashauri ya Mji Mbulu kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele.
Bw. Bosco Addo Ndunguru amehamishwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Musoma kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi.
Bw. Hassan Nyange amehamishwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Mbulu.
Bw. Khalid Khalif amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.
Dkt. Peter Maiga Nyanja amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Makambako.
Bi. Anastazia Tutuba Ruhamvya amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Musoma.
Bi. Kuruthum Amour Sadick amehamishwa kutoka Halmashauri ya Mji Njombe kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga.
Bw. Sajidu Idrisa Mohamed amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Madaba kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa.
Bw. Abdallah Nandonde amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala.
Bw. Emmanuel Johnson Matinyi amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe.
Bw. Anderson Msumba amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mtama kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Njombe.
Bi. Hanan Mohamed Bafagih amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.
Bw. Christopher Aloyce Sanga amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Njombe kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi.
Bw. Kenneth Kenneth Haule amehamishwa kutoka Halmashauri ya Mji Makambako kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama. (Angalia ufafanuzi zaidi chini)
D. Ufafanuzi Kuhusu Uteuzi na Uhamisho (Nyongeza)
Kufuatia taarifa hiyo, kuliwekwa wazi ufafanuzi kuhusu uteuzi na uhamisho uliotolewa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 29 Septemba, 2026, ambao unasomeka kama hivi:
Bi. Sigilinda Modest Mdemu amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mlele kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.
Bw. Anderson David Msumba amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mtama kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Njombe.
Bw. Kenneth Kenneth Haule amehamishwa kutoka Halmashauri ya Mji Makambako kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.
Uteuzi na uhamisho huu unaanza mara moja.

Post a Comment