MISS WORLD 2027 ITAKUWA YA KIPEKEE
Mashindano ya Miss World 2027 yanayotarajiwa kufanyika nchini yanatarajiwa kuwa ya kipekee kwa kuzingatia utamaduni na maadili ya jamii, hususan katika kipengele cha mavazi ya heshima (Modesty).
Waziri wa Maliasili na Utalii wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Nasra Nassor Omar, amesema katika mazungumzo na uongozi wa Miss World Organization amesisitiza umuhimu wa kuwa na mavazi yanayomstiri mwanamke huku yakionesha utambulisho na utajiri wa tamaduni za mataifa mbalimbali.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Novemba 20, 2026, Zanzibar, amesema hatua hiyo itatoa nafasi ya kuifanya Miss World kuwa jukwaa la kuonesha uzuri wa mavazi yenye heshima bila kupoteza upekee wa mashindano hayo.
Ameongeza kuwa mashindano hayo pia yatatumika kuhamasisha uhifadhi wa mazingira na bahari kupitia programu za Green Zanzibar na Miss Oceanic, sambamba na kuitangaza Tanzania kimataifa.
Post a Comment