Mustafa aomba Watanzania kumpigia kura Latricia




 Mkurugenzi wa Miss World Tanzania, Mustafa Hassanali aliwaomba Watanzania kumpigia kura Latricia awamu ya kwanza shindano la chaguo la watu. 

Hassanali alisema washindi wa chaguo la watu wa kila bara wataingia moja kwa moja kwenye fainali ya 40 bora. 

“Huu ni wakati wetu wa kusimama pamoja na kuifanya sauti ya Tanzania isikike,” alisema Hassanali. 

Ili kupiga kura, unaingia kwenye kiunganishi kwenye wasifu wa Miss World au changanua msimbo wa QR kwenye bango kisha piga kura yako.

“Hebu tumsukume Latricia tangu mwanzo kwani kila kura inahesabiwa. Kila sauti ni muhimu. Tufanye hivyo, Tanzania,” aliongeza. 

Shindano la 73 la Miss World linaendelea nchini Vietnam tangu Agosti 9 na fainali zitakazofanyika Septemba 5, mwaka huu.

Wakati huo huo Miss World Tanzania, Latricia Ian ameshiriki kipengele cha Top Model Competition kwenye jukwaa la Miss World 2026 akiendelea na safari yake ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo yanayoendelea nchini Vietnam. 

Latricia aliteka hisia za wengi kwa kutembea kwa madaha mithili ya Twiga, huku akionesha utulivu na kujiamini kwa hali ya juu huku akitamba kwa madaha akiwa amevaa gauni jeupe la kifahari lililopambwa kwa mapambo yanayong’ara na kumfanya amulike jukwaani .


No comments