Latricia aanza vizuri Miss MISS World Tanzania 2026




Latricia Ian ameonekana katika vazi la kuvutia la rangi ya pinki na fedha wakati wa hafla ya utambulisho ya mashindano ya Miss World 2026 nchini Vietnam. 

Gauni hilo limebuniwa na mbunifu wa Tanzania, Queens Abdallah ‘Indeity’ likiwa na mwonekano unaoonesha uzuri, hadhi na kujiamini. 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Latricia amesema vazi hilo limeakisi uzuri na kujiamini, huku likimsaidia kuiwakilisha Tanzania kwa fahari kwenye jukwaa la Miss World 2026. 

Pia, alifanya vizuri katika hafla ya kuvaa rasmi utepe wenye jina la nchi ambayo anaiwakilisha ambayo ni hatua muhimu kuelekea mashindano ya Miss World 2026, hatua iliyofanya kupongezwa na wadau kwa jinsi alivyoonesha heshima wakati akivalishwa utepe. 

Katika hafla hiyo, Latricia amevalia gauni jekundu World 2026 lililobuniwa na Seamy Luxe, likiwa sehemu ya muonekano wake wa kuiwakilisha Tanzania mbele ya washiriki na wageni kutoka mataifa mbalimbali. 

Baada ya kuvishwa utepe huo, Latricia anaendelea na ratiba rasmi za Miss World 2026, akiiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo ya kimataifa kupitia kaulimbiu: ‘Beauty With A Purpose’. 

Mashindano yote yanafanyika nchini Vietnam, huku sherehe za ufunguzi zikifanyika katika Mkoa wa Quang Ninh. Latricia anachuana akitumia mradi wake wa kijamii ujulikanao kama ‘Nuru ya Elimu kwa Usonji’ unaolenga kusaidia watoto wenye ugonjwa wa usonji. 

Baada ya uzinduzi warembo jana walitembelea vivutio, leo watafanyiwa mchujo wa shindano la vipaji, Agosti 17 shindano la mapishi, Agosti 18 ni shindano la wanamitandao bora Agosti 19 mashindano ya michezo

No comments