VIJANA KAGERA WACHAGUA AMANI
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Kagera, Faris Buruhani, amesema kaulimbiu mpya ya vijana wa mkoa huo ni “Kagera Tumechagua Amani”, akisisitiza kuwa amani na utulivu ni msingi wa maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.Faris amesema hayo alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Kilimo na Mifugo Igabiro, Kata ya Biirabo wilayani Muleba, ambapo ametoa wito kwa vijana kuendelea kulinda amani, mshikamano na umoja katika jamii.
Ameeleza kuwa hakuna maendeleo ya kiuchumi, kijamii au kielimu yanayoweza kupatikana bila kuwepo kwa mazingira ya amani na utulivu, hivyo vijana wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kuitunza tunu hiyo muhimu.
Aidha, amewahimiza wanafunzi kutumia elimu wanayoipata kujitengenezea ajira na kuchangia maendeleo ya taifa, sambamba na kutumia fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya kuwawezesha vijana kiuchumi.

Post a Comment