David Jonsson Atangazwa Kuwa T’Challa Mpya Katika ‘Black Panther III’



Mwigizaji mahiri wa filamu za kimataifa, David Jonsson—anayefahamika zaidi kupitia kazi zake kali kwenye filamu za ‘The Long Walk’, ‘Rye Lane’ na ‘Alien: Romulus’—ametangazwa rasmi kuigiza nafasi ya T’Challa II, mtoto wa marehemu Mfalme T’Challa, katika filamu inayotarajiwa kwa hamu kubwa ya Black Panther III, ambayo imepangwa kutoka rasmi tarehe Desemba 15, 2028.

Tangazo hili kubwa limetolewa na mwongozaji mkuu wa filamu hiyo, Ryan Coogler, wakati wa tukio kubwa la San Diego Comic-Con 2026, alipomtambulisha Jonsson mbele ya umati akichukua rasmi usukani wa kuongoza awamu hii ya tatu ya franchise hiyo pendwa. 

Uamuzi huu unakuja takribani miaka sita tangu kutokea kwa kifo cha ghafla cha mwigizaji nguli Chadwick Boseman, ambaye aliifanya nafasi ya T’Challa na Black Panther kuwa ya kipekee duniani kabla ya kufariki dunia mnamo Agosti 2020 kutokana na saratani ya utumbo mpana.

Kwenye filamu hii mpya, Jonsson atacheza uhusika wa mtoto wa Mfalme T’Challa—ambaye hapo awali alitambulishwa kama mtoto mdogo anayeitwa Toussaint kwenye eneo la mwisho la filamu ya ‘Black Panther: Wakanda Forever’—akiwa sasa amekua na kuanza safari nzito ya kukabili changamoto na kurithi kiti cha enzi cha Wakanda. 

Wakati huo huo, mashabiki watafurahi kuona nyuso za baadhi ya waigizajipendwa wakirudi, ambapo Letitia Wright atarejea tena katika uhusika wake kama Shuri, na Winston Duke ataendelea kuonekana kama M’Baku.

No comments