RAIS SAMIA AVUNJA BODI YA WADHAMINI PSSSF
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amevunja rasmi Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).
Kuvunjwa kwa Bodi hiyo iliyozinduliwa Machi 27,2025 na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete, kumetangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka.
Bodi hiyo iliongozwa na Bi. Joyce Mapunjo kama Mwenyekiti, akisaidiana na CPA Pius Meneno ambaye alihudumu kama Makamu Mwenyekiti. Wajumbe wengine wa bodi hiyo walikuwa ni Bi. Emma Lyimo, Dkt. Haphsa Hincha, Bw. Tumaini Nyamhokya, Bi. Suzanne Doran, Bi. Vicky Jengo, pamoja na Bw. Sadi Shemliwa.

Post a Comment