MAKONDA ASAINI HATI YA MAKUBALIANO UENDESHAJI AFCON 2027 – MOTSEPE ASHUHUDIA
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda (Mb), leo amesaini hati ya makubaliano ya uendeshaji wa mashindano ya AFCON 2027, inayojulikana kama CAF Joint Resolution Total Energies.
Tukio hilo la kihistoria limeshuhudiwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Dkt. Patrice Motsepe, jijini Nairobi, nchini Kenya.
Hatua hiyo inalenga kuimarisha uratibu na ushirikiano katika maandalizi ya mashindano makubwa ya soka barani Afrika.
Aidha, katika mazungumzo hayo, wamejadili hatua muhimu kuelekea mashindano ya AFCON 2027, ikiwamo tathmini ya hatua iliyofikiwa na nchi katika maandalizi, utayari wa kitaifa, pamoja na maendeleo ya miundombinu inayohitajika.
Vilevile, Serikali imewasilisha ombi kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kutumia lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi katika mashindano hayo ya mwaka 2027.
Mkutano huo ulijumuisha mawaziri kutoka nchi tatu wenyeji wa AFCON 2027, Kenya, Uganda na Tanzania, pamoja na wenyeviti wa kamati za maandalizi za AFCON (LOC), Marais wa mashirikisho ya mpira wa miguu ya nchi hizo, pamoja na wataalamu wengine kutoka wizara za michezo katika nchi waandaaji.
Post a Comment