Bia ya Safari mdhamini rasmi Kombe la Dunia la FIFA 2026
Na Mwandishi Wetu
Bia ya Safari imezindua toleo maalumu la bia zenye ujazo wa ml 375 na ml 500 zenye lebo rasmi ya Kombe la Dunia la FIFA 2026, kama ishara ya fahari ya mafanikio makubwa ya kuwa mdhamini Kombe la Dunia la FIFA 2026.
Kwa mafanikio hayo Safari inakuwa chapa ya kwanza ya bia kutoka Tanzania kupata nafasi kwenye jukwaa kubwa zaidi la soka duniani.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL), Khensani Mkhombo alisema hiyo ni hatua kubwa inayowahusu mashabiki wote wa soka nchini ambao wameendelea kuamini na kuishi na mchezo wa soka kwa moyo wao wote.
Alisema udhamini wa Kombe la Dunia si jambo la bahati, bali ni matokeo ya safari ndefu ya uwekezaji na imani katika mchezo wa soka.
Kwa mara ya kwanza, chapa ya bia inaweka mashabiki katikati ya simulizi la soka na kuwapa nafasi ya kuthaminiwa kwa mchango wao, mapenzi yao na imani waliyoendelea kuonesha kwa miaka mingi.
“Bia ya Safari siku zote imeamini kuwa mabingwa hawapatikani uwanjani pekee. Ni mashabiki wanaojitokeza kila wakati, wanaouhisi kila mchezo ndani ya mioyo yao na ambao hawajawahi kuacha kuamini.
“Kwa zaidi ya miaka 40 tumekuwa pamoja nao, na leo tunajivunia kuwapa heshima wanayostahili kwenye jukwaa kubwa zaidi la soka duniani. Hii ni kwa ajili yao” alisema Mkhombo.
katika kuonesha fahari yake Bia ya safari Jumamosi ijayo itaendelea kuandika historia kupitia uzinduzi mkubwa utakaofanyika Mwenge, Dar es Salaam.
Mashabiki wanahimizwa kufuatilia kurasa rasmi za Safari Lager kwenye mitandao ya kijamii kwa taarifa zaidi kuhusu tukio hilo.
Michuano ya Kombe la Dunia itakapoanza, Safari Lager itaandaa maeneo mbalimbali ya kutazama mechi kote nchini ili kuwaleta mashabiki pamoja na kuwapa burudani, hamasa na uzoefu wa kipekee wa soka.
Kupitia kampeni ya “Mabingwa Wanastahili – Shinda Kibingwa,” mashabiki pia watapata nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali.
Ili kushiriki, mashabiki wanatakiwa kununua Safari Lager, kuangalia namba ya siri iliyo chini ya kizibo na kuituma kwa SMS kwenda namba 15067 ili kupata nafasi ya kushinda Smart TV au muda wa maongezi papo hapo.
Droo za kila wiki zitaonyeshwa mubashara kila Jumapili saa 11 jioni kupitia TBC1 katika kipindi cha Mabingwa Wanastahili,Shinda Kibingwa.
Fainali za Kombe la Dunia zinafanyika nchini Marekani, Mexico na Canada kuanzia Juni 11 hadi Julai 19 mwaka huu zitashuhudia Afrika ikiwa na timu 10 kwa mara ya kwanza ambazo ni Senegal, Algeria, Tunisia, Misri, Ivory Coast, Ghana, Cape Verde, Afrika Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Morocco.
Mwisho
Post a Comment