BENKI YA DUNIA YAELEZA IMANI KWA MUSTAKABALI WA TANZANIA NA AJENDA YA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050
Tarehe 18 Mei, 2026, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, alimpokea Ikulu jijini Dar es
Salaam, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayemaliza muda wake, Bw. Nathan
Belete, aliyefika kumuaga Mheshimiwa Rais na kumtambulisha mrithi wake, Bw.
Firas Raad.
Katika mazungumzo yao, Bw. Belete—aliyekuwa akisimamai
Tanzania, Malawi, Zambia na Zimbabwe, na ambaye sasa amepandishwa kuwa Mkurugenzi
wa Programu za Kikanda wa Benki ya Dunia barani Afrika—pamoja na Bw. Raad,
walizungumzia safari ya maendeleo ya Tanzania, matarajio ya nchi kwa siku
zijazo, na mwendelezo wa ushirikiano kati ya Tanzania na Benki ya Dunia.
Katika mahojiano haya, Bw. Belete anaeleza uzoefu wake,
mambo muhimu aliyojifunza na mtazamo wake kuhusu fursa za Tanzania kwa miaka
ijayo, huku Bw. Raad akieleza matarajio yake na maeneo ya kipaumbele anapoanza
majukumu yake nchini.
![]() |
BW. NATHAN BELETE, MKURUGENZI MKAZI WA BENKI YA DUNIA ANAYEMALIZA MUDA WAKE |
SWALI: Unapohitimisha kipindi chako cha miaka minne kama Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, ni mafanikio au hatua gani muhimu unazozikumbuka zaidi, hata sasa unapoanza jukumu jipya la kikanda barani Afrika?
JIBU: Ni
heshima kwangu kufanya kazi Tanzania, nchi nzuri yenye watu wazuri, kote Bara
na Zanzibar. Ni jambo lenye nafasi ya kipekee katika maisha yangu. Ninajivunia
ushirikiano wetu na Serikali, wananchi na wadau mbalimbali nchini, kupitia
programu kubwa inayogusa karibu sekta zote.
Katika kipindi changu, msisitizo ulikuwa zaidi kwenye
sekta zinazogusa maendeleo ya watu, hususan elimu, afya na hifadhi ya jamii.
Programu hizi zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Tunajivunia mchango wetu katika mageuzi ya sekta ya afya,
ikiwemo bima ya afya kwa wote, pamoja na maboresho ya elimu, hasa mitaala ya
shule za msingi na sekondari, na msukumo uliowekwa kwenye elimu ya ufundi na
stadi.
Pia ninafurahishwa na mageuzi yaliyofanyika kwenye
upande wa miundombinu, hasa katika sekta ya nishati.
Katika miaka ya hivi karibuni, tumeshuhudia Tanzania
ikipiga hatua kubwa katika upatikanaji wa nishati, halikadhalika katika sekta
ya maji na huduma za usafi wa mazingira vijijini; na matarajio yetu ni kuona
maeneo hayo yakiendelea kukua zaidi.
SWALI:
Tanzania inapojiandaa kuanza utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050
mwezi Julai 2026, ipi ni nafasi ya Benki ya Dunia katika kuunga mkono juhudi za
kuwapa vijana na sekta binafsi wajibu mkubwa zaidi katika mageuzi hayo?
JIBU:
Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ni fursa muhimu kwa Tanzania, ikichagizwa na
mwelekeo wa Serikali kwa vijana katika kukuza ajira na sekta binafsi, kama
msingi imara wa kuyafikia malengo ya Dira hiyo.
Kwetu sisi, Benki ya Dunia, tunaiona nafasi nzuri ya
kuvutia mitaji zaidi ya sekta binafsi ili kusaidia miradi mikubwa ya
miundombinu ikiwemo Reli ya SGR na maendeleo ya bandari.
Tunaamini haya yanawezekana, kwa kuwa Tanzania ni
miongoni mwa nchi zenye msingi wa uchumi imara barani Afrika, na mazingira
mazuri ya kuvutia uwekezaji wa sekta binafsi.
Kwa sababu hiyo, mageuzi katika mazingira ya biashara
na uwekezaji ni muhimu. Mengi yamefanyika, lakini bado kuna nafasi zaidi ya
kurahisisha uwekezaji wa sekta binafsi nchini.
Rasilimali za Tanzania zinaipa nchi nafasi ya kipekee, si
kwa ukuaji wake pekee, bali pia kwa maendeleo ya nchi jirani na kanda pana ya
Afrika.
Nafasi ya Tanzania kama kiungo cha nchi nane
zinazopakana nayo ni faida kubwa ya kuendelezwa. Kwa mtazamo wangu, hili ni
suala muhimu sana.
Namna tunavyotazama umuhimu wa vijana stereotypes na
nafasi yao katika maendeleo, tunagusa moja ya malengo makuu ya Benki ya Dunia
barani Afrika, ambalo ni kutengeneza ajira kwa vijana.
Nadhani njia hizi zinaweza kuwa msingi mzuri wa
kutengeneza ajira, sambamba na mageuzi ya mitaala ya elimu ya ufundi ambayo
tayari Tanzania imekwishaanza, yatasaidia kuwapatia vijana ujuzi na fursa bora
zaidi za ajira. Hili ni jambo muhimu sana kwa utengamano wa si tu Tanzania
pekee, bali bara zima la Afrika
SWALI:
Zaidi ya utajiri wa rasilimali za asili na utulivu wa kiuchumi, ni mambo gani
mengine yanayoifanya nchi ya Tanzania kuwa ya kipekee katika ukanda huu?
JIBU:
Tanzania ipo katika nafasi nzuri na ya kipekee ya ukuaji wa uchumi barani
Afrika. Ni nchi yenye utulivu, inayosimamia deni kwa umakini, na kutumia
rasilimali zake kwa weledi. Hata hivyo, bado kuna mwanya wa kufanya zaidi, na
kazi hiyo inaendelea. Katika majadiliano yetu kuhusu ufadhili wa Benki ya
Dunia, tumeshuhudia umakini wa Tanzania katika matumizi bora ya rasilimali
zilizopo.
Suala la msingi kwa sasa, ni mwelekeo wa kupunguza
utegemezi wa miradi inayofadhiliwa na sekta ya umma, na kuongeza miradi
inayofadhiliwa na sekta binafsi.
Jitihada hizi ni muhimu pia katika kuimarisha usimamizi
wa miradi, iwe ya sekta ya umma au binafsi; na niseme tunathamini hatua
zinazochukuliwa na Serikali katika eneo hili.
SWALI:
Katika kipindi ulichofanya kazi Tanzania, ni mambo gani muhimu umejifunza
utakayayaishi katika jukumu lako jipya la uongozi barani Afrika?
JIBU:
Mara kadhaa tumekuwa tukisema suala la utekelezaji ni changamoto kubwa barani
Afrika; lakini Tanzania, kwa mtazamo wangu, imeonesha kuwa sekta ya umma
inaweza kufanya kazi vizuri ikijizatiti.
Tumeshuhudia baadhi ya miradi yetu kutofanya vizuri
katika baadhi ya sekta, lakini pia tumeona matokeo makubwa katika sekta na
wizara nyingine.
Niliyoyaona Tanzania katika sekta ya nishati, maji
vijijini, pamoja na huduma za usafi wa mazingira yanavutia sana. Nchi hii
imeonesha kuwa utekelezaji wa miradi katika sekta muhimu na kuleta matokeo kwa
wananchi, ni suala linalowezekana.
Ningependa kuona kasi hii ya utekelezaji ikiendelea,
kwa sababu Tanzania imeonesha kuwa hilo linawezekana pale kunapokuwa Greeting
na dhamira na utayari kisiasa, kiutendaji, na uratibu kati ya wadau na jamii.
Hili ni moja ya masomo makubwa ninayoondoka nayo, na ninatumaini Tanzania
itaendelea kuimarisha uwezo wake wa utekelezaji katika wizara zote.
SWALI:
Kwa mtazamo wako, ni katika eneo lipi Tanzania inaweza kuweka msisitizo zaidi
ili kuongeza kasi ya maendeleo na kuhakikisha ukuaji wa uchumi unawanufaisha
wananchi wengi kwa muda mrefu?
JIBU:
Kuna maeneo machache ambayo, kwa mtazamo wangu, yanahitaji kuendelea kupewa
msisitizo. Kwanza, kunahitajika umakini zaidi katika ushirikishwaji wa wananchi
kwenye usanifu na utekelezaji wa programu mbalimbali.
Lakini pia panapaswa kuwa na uwazi na ufanisi zaidi
katika ushirikishwaji wa sekta binafsi. Mwisho, jitihada za kuimarisha utawala
bora zinapaswa kuendelezwa katika sekta zote, ili kulinda maslahi ya Taifa na
wananchi kwa ujumla.
![]() |
BW. FIRAS RAAD, MKURUGENZI MKAZI MPYA WA BENKI YA DUNIA |
SWALI: Kama Mkurugenzi Mkazi mpya wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, ni vipaumbele na fursa gani unazoziona katika hatua inayofuata ya ushirikiano kati ya Benki ya Dunia na Tanzania?
JIBU:
Leo, (Benki ya Dunia) tumepata heshima ya kukutana na Mheshimiwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kujadili mtazamo na matarajio yetu kuhusu
mustakabali wa ushirikiano wetu.
Nilieleza pia mtazamo wangu kuhusu kasi kubwa ya ukuaji
wa uchumi wa Tanzania na utulivu wa uchumi kwa ujumla. Mambo haya mawili ni
msingi muhimu wa maendeleo ya sekta binafsi tunayoyaona. Na ni maeneo ambayo
kimsingi tutaendelea kuyapa kipaumbele.
Kwa upande wetu sisi Benki ya Dunia, na hili
tulilieleza kwa Mheshimiwa Rais, pamoja na viongozi wa Serikali, ajenda ya
ukuaji wa uchumi na ajira ni suala muhimu sana.
Ili kufikia azma ya kupunguza umaskini kwa ufanisi,
tunahitaji si tu kukuza uchumi, bali pia kutengeneza ajira. Hili litasaidia
kufikia lengo la kupunguza umaskini na kuinua hali ya maisha ya Watanzania
wote.
Katika kufanikisha hilo, hatuna budi kuweka mkazo
katika miundombinu ya msingi, yaani miundombinu ya watu na vitu; ambayo ni
elimu, hifadhi ya jamii, na afya, pamoja na nishati, usafiri na mengineyo.
Hili, kwa mtazamo wangu, ni eneo muhimu sana.
Eneo la pili ni kuimarisha mazingira wezeshi ya
biashara, jambo ambalo Tanzania imeendelea kulifanyia kazi. Tunatarajia
kuendelea kushirikiana na Serikali, Tanzania Bara na Zanzibar, katika kujenga
mazingira yatakayovutia uwekezaji unaohitajika kuendeleza kasi ya ukuaji wa
uchumi.
Na mwisho, ni eneo ambalo Mkurugenzi anayemaliza muda
wake pia amelipa msisitizo, nalo ni kutumia mtaji wa sekta binafsi kuchochea
maendeleo. Tunahitaji nguvu zaidi kuiunga mkono Tanzania ili iweze kuvutia
mtaji wa sekta binafsi katika maeneo muhimu yanayoweza kubadili uchumi wa nchi.
Kama mnavyofahamu, nafasi ya fedha za umma kugharamia
mahitaji ya maendeleo imeendelea kuwa finyu. Ndiyo maana ni muhimu mtaji wa
sekta binafsi uingie kuongeza nguvu katika maeneo ambayo Serikali haiwezi
kuyagharamia peke yake.
Kwa hiyo, matarajio yetu ni kuendelea kushirikiana kwa
karibu na Serikali ya Tanzania, kupanua na kuimarisha ushirikiano huu, huku
tukihakikisha unaendelea kujikita katika maendeleo yanayomgusa mwananchi moja
kwa moja.
Ninatarajia kuendeleza ushirikiano huu katika jukumu
langu jipya kama Mkurugenzi wa Benki ya Dunia, ninayeisimamia si Tanzania
pekee, bali pia Malawi, Zimbabwe na Zambia.
SWALI:
Ni kwa namna ipi Benki ya Dunia inaweza kusaidia Tanzania na ukanda huu kwa
ujumla kuimarisha rasilimali watu, na kuwaandaa vijana kwa ujuzi unaohitajika
katika uchumi wa siku zijazo?
JIBU:
Kama mnavyofahamu, elimu ni sekta muhimu sana. Ni moja ya maeneo ambayo
uwekezaji wake huleta matokeo makubwa, ingawa matokeo hayo huonekana zaidi
katika muda wa kati na mrefu.
Kwa hiyo, tunahitaji kuwekeza sasa ili kuona matokeo
bora ya ujifunzaji katika miaka mitano hadi saba ijayo. Kwahiyo, Benki ya Dunia
inawekeza zaidi katika maendeleo ya watu, hususan elimu, hifadhi ya jamii na
afya.
Mtakumbuka kuwa, miaka michache iliyopita, Tanzania
ilikuwa mwenyeji wa Mkutano wa Rasilimali Watu, uliochangia kuweka msisitizo
mkubwa katika eneo hili na kuonesha nini kinaweza kufikiwa. Bado kuna mapengo
makubwa katika nchi nyingi barani Afrika, lakini kupitia uwekezaji katika
elimu, afya na hifadhi ya jamii, tunaweza kuanza kuyapunguza.
Jambo lingine muhimu ni ujuzi unaohitajika kwa ajili ya
nguvu kazi ya siku zijazo. Hatuwezi kuzisaidia nchi kukuza uchumi, kupunguza
umaskini na kuinua hali ya maisha ya wananchi bila kuboresha matokeo ya
ujifunzaji na ujuzi wa nguvu kazi. Hili pia ni eneo tunalotarajia kuendelea
kuiunga mkono Serikali ya Tanzania, pamoja na Serikali nyingine katika ukanda
huu.
SWALI:
Na je, katika kipindi cha muda mfupi, mambo yapi yapewe kipaumbele?
JIBU:
Katika kipindi cha muda mfupi, tunaweza kuongeza uwekezaji katika afya na
hifadhi ya jamii, kwa sababu ni muhimu kulinda rasilimali watu. Kama
mnavyofahamu, nchi nyingi barani Afrika mara kwa mara hukumbwa na misukosuko
kutoka nje, iwe ni athari za tabianchi au changamoto za kiuchumi, kama
tunavyoona sasa kutokana na mgogoro wa Mashariki ya Kati. Hivyo, tunahitaji
kuhakikisha uchumi wetu, na hata kaya zetu, zina uwezo wa kuhimili changamoto
hizo.
Hili linawezekana kupitia mifumo ya kisasa ya hifadhi
ya jamii na upatikanaji wa huduma bora za afya. Katika maeneo haya, tunajivunia
kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Tanzania.






Post a Comment