RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA WABUNGE SITA YUMO GWAJIMA, THABITI KOMBO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo amefanya uteuzi wa Wabunge sita wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akitumia mamlaka aliyonayo chini ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses M. Kusiluka, imesema uteuzi huo umefanywa kwa mujibu wa Ibara ya 66(1)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977.
Ibara hii ya Katiba inabainisha muundo wa Bunge na inampa Rais mamlaka ya kuteua idadi ya Wabunge wasiozidi kumi (10), ambao wanakuwa sehemu kamili ya Bunge la Jamhuri ya Muungano.
Wafuatao ndio Wateule wapya walioteuliwa na Rais Samia:
(i) Dkt. Dorothy Onesphoro Gwajima
(ii) Balozi Mahmoud Thabit Kombo
(iii) Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa
(iv) Bw. Abdullah Ali Mwinyi
(v) Balozi Khamis Mussa Omar; na
(vi) Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho.
Uteuzi huu unawaongeza Wabunge wapya katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Baadhi ya Wateule, kama Dkt. Dorothy Gwajima na Balozi Mahmoud Thabit Kombo, wanarejea katika nafasi hiyo.

Post a Comment