KESHO UAPISHO WA WAZIRI MKUU MTEULE, MHE. DKT. MWIGULU LAMECK NCHEMBA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, atamuapisha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb.) kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kesho, tarehe 14 Novemba, 2025 , Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma, saa 04:00 asubuhi.

Taarfifa ya uapisho imetolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Mpogole Kusiluka.

Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb.) ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan , na jina lake kuthibitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo, tarehe 13 Novemba, 2025 kwa kura 369 kati ya kura 371 , mbili zikiharibika.

No comments