TWIGA STARS YAFUZU WAFCON 2026 SASA YAKODOLEA MABILIONI YA CAF
Timu ya Taifa ya Soka ya Wanawake, 'Twiga Stars', imefuzu fainali za Kombe la mataifa ya Afrika kwa wanawake (WAFCON) 2026, kwa jumla wa mabao 3-0 dhidi ya Ethiopia.
Katika mchezo wa kwanza Dar es Salaam, Aisha Mnunka, mmoja wa nyota wa timu, alifunga bao la kuongoza mapema dakika ya 7, kabla ya Jamila Rajabu kuongeza la pili dakika ya 54.
Katika marudiano,mchezo uliopigwa uwanja wa kimataifa wa Dira Dawa, Twiga Stars walionyesha utulivu mkubwa. Kocha Bakari Shime, anayejulikana kwa nidhamu yake ya kiufundi, aliiweka timu yake imara licha ya shinikizo la Ethiopia na Tanzania ilipata bao katika dakika ya 60 kupitia kwa Diana Lucas, ambaye alikuwa ameingia uwanjani dakika chache tu kabla.
Hii ni mara ya pili mfululizo na ya tatu kwa Twiga Stars kufuzu michuano hii baada ya kufuzu mwaka 2010 na 2024 ambazo zilichezwa Juni mwaka huu Morocco.
Ushindi huu wa uhakika unaonyesha maendeleo makubwa ya timu yenye malengo, ambayo sasa imezoea kutawala katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Kwa kuangalia safari ya Twiga Stars utaamini kuwa Kocha Mkuu Bakari Shime na Nahodha Mkuu Opa Clement wamefanikiwa kuiwezesha timu kutinga fainali za WAFCON kwa mara ya tatu kwenda kuwania fuba kubwa zaidi. Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limenogesha zawadi mashindano hayo kufikia Dola za Marekani milioni 1, jambo linalofanya ushiriki wa Twiga Stars kuwa wa thamani zaidi.
Kuanzia WAFCON ya 2024 (ambayo ilikuwa imechezwa kabla ya kufuzu kwa 2026), CAF iliongeza fedha za zawadi (Prize Money) kwa mshindi kwa 100% na jumla ya fedha zote za zawadi kwa 45%.
Akizungumza kuhusu ongezeko hilo, Rais wa CAF, Dk. Patrice Motsepe alisema, "CAF inaendelea na dhamira yake ya kuendeleza na kukuza Soka la Wanawake barani Afrika. Ongezeko hili linapaswa kuchangia katika kuongeza mishahara ya Wachezaji, makocha, na wafanyakazi wa Soka la Wanawake."
Mshindi wa kwanza ataondoka na Dola za Marekani 1,000,000;Mshindi wa Pili Dola za Marekani 500,000; Nafasi ya Tatu Dola za Marekani 350,000; Nafasi ya Nne Dola za Marekani 300,000, huku timu zilizofika Robo Fainali zikipwatia dola za Marekani 200,000 (kwa kila timu).
Timu ya 3 Kwenye Kundi atapatiwa dola za Marekani 150,000 na Timu ya 4 Kwenye Kundi (3) atapata dola za Marekani 125,000 (kwa kila timu)
Kwa mujibu wa Cafonline jumla ya zawadi zote hizo ni dola za Marekani 3,475,000.
Muundo wa Mashindano na Timu Zilizofuzu
Mashindano ya mwisho yamepangwa kwa makundi matatu (3) yenye timu nne (4).Timu mbili za juu kutoka kila kundi, pamoja na timu mbili (2) bora zilizoshika nafasi ya tatu, zitafuzu moja kwa moja kwa Robo Fainali.Kutoka hapo, mashindano yanaendelea kwa mfumo wa mtoano hadi Fainali.
Nchini Morocco,Twiga Stars itajiunga na mataifa mengine yaliyofuzu ambayo ni Morocco (Mwenyeji) Zambia, Tanzania, Malawi, Algeria, Nigeria, Ghana, Burkina Faso na Kenya.

Post a Comment