KAMATI ya
rufaa ya maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imetupa rufaa ya
aliyekuwa makamu wa Rais wa TFF, Michael Wambura kufungiwa maisha kujihusisha
na shughuli za soka.
Akisoma hukumu
hiyo leo Mwenyekiti wa Kamati ya maadili ya TFF, Ebenezer Mshana alisema
kamati yake ilipitia hukumu tatu ambazo zilikatwa kwa kamati hiyo dhidi ya TFF.
Mshana
alisema baada ya kupitia hukumu zote tatu na hoja za rufaa, rufaa moja ya Edgar
Chibula ilishinda na rufaa mbili ambazo ni ya Wambura na Dustan Mkundi kamati imejiridhisha
na maamuzi ya awali yaliyotolewa na kamati ya maadili kuwafungia maisha.
“Upande wa
utetezi wa Wambura ambao ulikuwa na mawakili watatu ukiongozwa na Masumbuko
Lamwai ulileta mbele ya kamati hoja nne za kupinga mteja wao kufungiwa maisha
kujihusisha na soka na upande wa TFF uliwakilishwa na wanasheria wawili
ikiongozwa na Allan Kiluvya,” alisema Mshana.
“Katika
barua yake ya Desemba4, 2016 kamati ya maadili ya rufaa imejiridhisha kuwa
Wambura alipewa nafasi ya kujieleza kwani alitakiwa kufanya na kamati ya
ukaguzi na ushahidi wa video uliwasilishwa mbele ya kamati hiyo,” alisema
Mshana
Katika hoja
za rufaa kamati ilisikiliza pande zote mbili za rufaa na upande uliokatiwa
rufaa ambao ni TFF baada ya kusikiliza pande zote mbili kamati ilijiridhisha na
maamuzi ya kamati ya maadili.
Kamati ya TFF ilimfungia
kujihulisisha na soka maisha Makamu wa Rais wa TFF, Michael Wambura baada ya kumkuta na hatia katika tuhuma tatu
zilizokuwa zinamkabili kwa mujibu wa Kifungu cha 73(1)(c)
cha Kanuni za Maadili ya TFF toleo la 2013 kama zilivyofikishwa kwenye kamati
na sekretarieti ya TFF.
Wambura alifikishwa
kwenye kamati ya maadili na sekretarieti ya TFF kwa makosa ya kupokea/kuchukua
fedha za TFF kwa malipo yasiyo halali halali na kughushi barua ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(1) cha Kanuni
za Maadili za TFF Toleo la 2013.”
Kufanya vitendo
vinavyoshusha hadhi ya Shirikisho ikiwa ni kinyume na ibara ya 50(1) ya Katiba
ya TFF (kama ilivyorekebishwa 2015)
Kamati ya
rufaa ya maadili imeiagiza TFF kulifikisha suala la Wambura na Danstun Mkundi
kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa hatua zingine za kisheria na imebariki
kifungo cha maisha cha kutojihusisha na soka maisha
Kwa upande
wa wakili wa Wambura, Emanuel Muga alisema mteja wake hajaridhishwa na hukumu
hiyo hivyo amesema atakata rufaa katika ngazi nyingine.
No comments:
Post a Comment