WAIGIZAJI wa Tanzania, Wema Sepetu na Salim Ahmed ‘Gabo’ juzi waliwatoa kimasomaso
Watanzania baada ya kuibuka waigizaji bora katika tuzo
za filamu za Sinema Zetu International Film Festival Award (SZIFF)
zilizofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam
Katika filamu hizo ambazo zilikuwa na vipengele 19 ambavyo vilikuwa vinawania
kimoja kikiwa kipengele cha chaguo la watu ambapo Gabo alichukua tuzo tano na Wema
Sepetu aliondoka na tuzo mbili na filamu ya ‘Binti Zanzibar’ kutoka Zanzibar ikiondoka
na tuzo tatu.
Gabo ambaye
aliingiza filamu ya Safari ya Gwalu aliondoka na tuzo ya mwigizaji bora wa
kiume ambapo pia Safari ya Gwalu ilipata tuzo ya filamu bora, skiripti bora, muziki
bora wa filamu pia ikapata tuzo ya mwongozaji bora, (Daniel Manege)
Wema alipata
tuzo ya mwigizaji bora wa kike na filamu yake ya Heaven Sent ikapata tuzo ya
watazamaji kwani ilipigiwa kura na watazamaji.
Filamu ya
binti Zanzibar iliondoka na filamu tatu katika vipengele vya filamu fupi bora, best Screen Play na Best Original Music (Abdallah Marash)
Mchekeshaji bora alikuwa Musa Kitale, mhariri bora wa filamu Soudy Visual (Usinitege), mwongozaji bora wa filamu Said Abdallah (Picha) na sinematografia bora ni Usinitege iliyotengenezwa na Soudy Visual
Filamu bora ni malipo duni kwa wapagazi na mwongozaji bora ni Anwar Msechu kupitia filamu ya malipo duni kwa wapagazi
Mchekeshaji bora alikuwa Musa Kitale, mhariri bora wa filamu Soudy Visual (Usinitege), mwongozaji bora wa filamu Said Abdallah (Picha) na sinematografia bora ni Usinitege iliyotengenezwa na Soudy Visual
Filamu bora ni malipo duni kwa wapagazi na mwongozaji bora ni Anwar Msechu kupitia filamu ya malipo duni kwa wapagazi
Filamu ya Watatu kutoka Kenya iliondoka na tuzo ya mhariri bora wa filamu
na sinematografia bora.
Akizungumza baada ya kukabidhi tuzo mgeni rasmi Rais
Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Kikwete ambaye aliwataka wasanii kutumia
fursa hiyo kutengeneza kazi nzuri ambazo zitaweza kushindana kimataifa na
kuacha kuiga wasanii wa nje.
Tuzo hizo zilihudhuriwa na wasanii na watu maarufu wengi akiwemo mwigizaji
kutoka India aitwaye Pritika Rao maarufu kama Aliyah ambaye amejizolea umaarufu
kupitia tamthilia ya ‘Beitehaa’ Mzee Majuto, Naibu Waziri wa Habari, Sanaa,
Michezo na Utamaduni Juliana Shonza na Katibu Mkuu wa bodi ya filamu Joyce
Fissoo
Mchakato wa
kupata mshindi wa tuzo hizo ulianza Oktoba mwaka 2017 ambapo mwigizaji
Elizabeth Michael ‘Lulu‘ alichaguliwa kuwa balozi wa (SZIFF) Sinema Zetu
International Festival kwa mwaka 2017/2018.
No comments:
Post a Comment