MULTICHOICE YAITISHA MAFUNZO KWA WAHITAJI YA UTENGENEZAJI FILAMYU



Taasisi ya mafunzo ya filamu na televisheni ya Afrika , MultiChoice Talent Factory (MTF), imefungua rasmi maombi ya wadau wa filamu wenye ndoto ya kuwa waongozaji, watengenezaji filamu, waandishi wa miswada, watayarishaji, na wasimulizi wa hadithi.

Mafunzo hayo yatafadhiliwa kikamilifu na  MTF.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari wahitaji wanaweza kuomba kujiunga na kozi zinazofadhiliwa kikamilifu .

Taarifa imesema kwamba kwa  kuwa sehemu ya CANAL+ hivi karibuni, MultiChoice imejitolea upya kuleta programu zinazovutiana njia moja kuu ya kufanya hivyo ni kwa kuwawezesha vijana kupata ujuzi wa utengenezaji filamu, utayarishaji, na usimulizi wa hadithi. 

Taarifa imesema mafunzo hayo ni ya miezi tisa  yatatolewa kwa mfumo mseto (hybrid), ukichanganya masomo ya mtandaoni yenye mwingiliano na mafunzo ya ana kwa ana (in-person training).

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2018, MTF imefunza watengenezaji filamu 296, huku zaidi ya filamu 42 zikizinduliwa na wahitimu wake.  Washiriki wanatakiwa kutayarisha miradi yao ya filamu, ambayo huonyeshwa baadaye kwenye chaneli za DStv na GOtv—ikiwemo Maisha Magic, Zambezi Magic, na Africa Magic—pamoja na kwenye jukwaa la kutiririsha la Showmax.

Baada ya kuhitimu, viwango vya mafanikio vya wahitimu ni vikubwa. Wengi huendelea kufanya kazi ndani ya mfumo wa MultiChoice, wakisaidia kuunda matayarisho makuu ya Kiafrika. Uidhinishaji wa MTF huwafanya wahitimu kutafutwa sana, na wengi wameanzisha miradi yao wenyewe; hadi sasa, zaidi ya kampuni 50 za utayarishaji zimeanzishwa na wahitimu wa MTF.

Baadhi ya wahitimu wa MTF wameshiriki na kushinda tuzo nyingi kwenye Africa Magic Viewers’ Choice Awards (AMVCA), Kalasha Awards, Uganda Film Festival, na Women in Film Awards. Pia, wahitimu hufanya kazi na wabunifu katika maeneo ya kimataifa, ikiwemo European Film Market na Durban FilmMart.

Kwa kujisali kupata mafunzo hayo tembelea https://multichoicetalentfactory.com/mtf-applications/index.php ili kupata maelezo zaidi kuhusu mahitaji ya programu ya MTF.Maombi yatafungwa tarehe 27 Februari 2026.

No comments