LIGI ya
mabingwa wa mikoa inatarajiwa kuanza Mei Mosi hadi Mei 18 na imepangwa
kufanyika katika vituo vinne na itashirikisha timu 28.
Akizungumza
na wandishi wa habari leo, Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) Efrem August alisema ligi hiyo itachezwa katika vituo vya
Kilimanjaro, Rukwa, Singida, na Geita.
“Mikoa ya
Geita, Kilimanjaro, Singida na Rukwa ndio itakuwa mwenyeji wa vituo na kila
kituo kitakuwa na timu saba. Pia hii mikoa ambayo imepata wenyeji ilikubali
kugharamia malazi na chakula kwa waamuzi, kamishna na wasimamizi wa vituo,” alisem
Efrem.
Kituo D cha
Kilimanjaro kitakuwa na timu za Karume Market ya Dar es Salaam, Sahare ya
Tanga, Bishop Durning Sports ya Arusha, Usalama Sports Club ya Manyara, Stand
FC ya Pwani, Moro Kids ya Morogoro na Uzunguni FC ya Kilimanjaro
Kituo C cha
Singida kitakuwa na timu za Gwassa Sports ya Dodoma, Iringa United ya Iringa, Kipagalo
FC ya Njombe, Temeke Market ya Dar es Salaam, Majimaji Rangers ya Lindi, Mwena
FC ya Mtwara na wenyeji Stand Dortmund ya Singida.
Kituo B cha
Rukwa kitakuwa na timu za Watu FC ya Katavi, Laela FC ya Rukwa, Tukuyu stars ya
Mbeya, Red Stars FC ya Kigoma, Tabora FC ya Tabora, Black Belt ya Ruvuma na
Migombani FC ya Songwe
Kituo A
kitakuwa Geita na timu za Ungindoni ya Dar es Salaam, Kumunyange FC ya Kagera,
Fathom FC ya Mwanza,Zimamoto FC ya Shinyanga, Nyamongo ya Mara, Gipco FC ya
Geita na Ambassador FC ya Simiyu.
Usajili
ulifungwa jana na Aprili 24 kutafanyika
kikao cha kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji baada ya kamati ua usajili na pingamizi
kukutana Aprili 18
No comments:
Post a Comment