TIMU ya
Wanawake ya Soka ya Tanzania Twiga
Stars, imeaga mashindano ya Afrika kwa wanawake baada ya kutoka sare ya bao 1-1
kwenye mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Nkoloma Lusaka Zambia.
Mchezo huo
wa kutafuta kufuzu fainali za Afrika zinazotarajiwa kufanyika Ghana kuanzia Novemba 17 hadi Desemba Mosi mwaka huu jahazi la Twiga
lilionekana kuanza kuzama mapema baada ya kukubali bao la mapema.
Wenyeji She
Polopolo walipata bao dakika ya tatu lililofungwa na Rachael Kundanaji baada ya
kumzidi mbio beki Sophia Mwasikili na kudumu hadi mapumziko licha ya kutawala
mchezo kipindo chote hicho.
Twiga Stars ambao
walitawala mchezo kipindi cha pili walisawazisha bao hilo dakika ya 71 ambalo
lilifungwa na mshambuliaji Donisia Daniel akiunganisha kona iliyopigwa na
Mwanahamisi Omar ’Gaucho’
Kwa matokeo
hayo Zambia wamefuzu hatua ya pili kwa ushindi wa mabao 4-4 baada ya kutoka
sare ya mabao 3-3 nyumbani na sasa itakutana na mshindi kati ya Zimbabwe au
Namibia.
Twiga Stars
iliwahi kufuzu fainali hizo 2010 ambazo zilifanyika nchini Afrika Kusini na
kutolewa katika hatua ya makundi.
No comments:
Post a Comment