TIMU ya Taifa ya Soka ya Wanawake ya Twiga
Stars imeshindwa kuutumia vizuri uwanja wao wa nyumbani baada ya
kulazimishwa sare ya kufungana mabao 3-3 na wenzao wa Zambia, katika mchezo
uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo ni kwa ajili ya kufuzu kucheza
fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Ghana baadaye mwaka huu.
Twiga Stars iliandika bao la kwanza katika
kipindi cha kwanza baada ya Stumai Abdallah kufunga bao na kuifanya timu hiyo
kuwa mbele baada ya kupokea pasi ya Asha Rashid.
Twiga Stars iliandika bao la pili kupitia kwa
Asha Rashid aliyefunga katika dakika ya 22 baada ya kuiwahi krosi ya chini
chini iliyochongwa na Stumai Abdallah.
Dakika tano baadaye, Zambia waliandika bao la
pili kupitia kwa mshambuliaji wao hatari Barbra Banda katika dakika ya 27 kabla
ya timu hiyo haijasawazisha katika dakika ya 49 kupitia kwa Misozi Zulu.
Twiga Stars ilipata bao la tatu lililofungwa
na Asha Rashid katika dakika ya 47 kwa shuti kali lililomshinda kipa wa timu ya
taifa ya Zambia, Catherune Chileshe.
Zambia walisawazisha kupitia kwa mchezaji wao
hatari, Banda baada ya kuwapiga chenga karibu mabeki wanne wa Twiga Stars na
kuujaza mpira kimiani.
Kikosi cha Tanzania:
Fatuma Omary, Wema Richard, Happy Hezron, Fatuma Issa, Sophia Mwasikili/Ester
Mayala, Everline Sekikubo, Stumai Abdallah, Donisia Daniel, Asha Rashid,
Mwanahamisi Omary na Amina Ally.
No comments:
Post a Comment