KLABU ya Simba leo imeandika historia katika soka la Tanzania baada ya kukubali na kuingia rasmi katika mfumo wa hisa baada ya mfanyabiashara Mohamed Dewji ‘Mo’ kutangazwa mshindi wa zabuni ya kuweza kwa dau la Sh. Bilioni 20.
Akizungumza
wakati akitangaza mchakato wa Jaji Mstaafu Thomas Mihayo alisema kuwa Mo ndiye
mwekezaji pekee aliyejitokeza kuomba zabuni hiyo baada ya kutangazwa na kukidhi
vigezo vyote vilivyowekwa.
“Mfanyabiashara
Mohamed Dewji ‘Mo’ amepita katika mchakato wa awali wa uwekezaji wa klabu ya
Simba kwa kukubaliwa kuwekeza Sh. Bilioni 20 kwani alikuwa mwombaji pekee
aliyetuma maombi katika kamati yetu na ndiye mshindi wa tenda kwani ametimiza
vigezo vyote,”.
“Tumejiridhisha
kupitia Kamati Maalumu ya kutathimini Zabuni, lakini pia tunaangalia jinsi gani
ataweza kulipa madeni ya klabu yaliyopo sasa, kodi zinazodaiwa na TRA na hatima
ya michezo mingine kwani majadiliano zaidi yatafanyika baada ya mkutano wa leo
(jana),” alisema Jaji Mstaafu Mihayo
Jaji Mihayo
alieleza kuwa mwekezaji huyo atakuwa akiweka wazi mipango yote ya klabu ikiwemo
kusajili wachezaji, kuajiri benchi la ufundi, kutengeneza viwanja vya mazoezi,
gym, hosteli ya wachezaji, kuanzisha akamemi, bwawa la kuogelea na jengo la
ofisi za klabu.
Pia alisema mwekezaji
ameeleza jinsi ya kuwa na vyanzo vya mapato kwa klabu ikiwemo mapato ya getini,
kodi za majengo, riba za fedha zitakazokuwa benki, uuzaji wa jezi, kofia na
mengineyo.
Akizungumza
baada ya kutangazwa Mo aliweka wazi ahadi kumi ambazo atatekeleza kuwa ni Kujenga
viwanja viwili bora ambavyo vitakuwa na nyasi asilia na nyasi bandia, Kujenga
hosteli ya wachezaji na benchi la ufundi yenye vyumba 35
Kujenga
mgahawa kwa ajili ya wachezaji, kujenga gym na bwawa la kuogelea kwa ajili ya
wachezaji, kujenga kituo cha kulea vijana chini ya umri wa miaka 14, 16, 18
Kurejesha
Simba katika historia ya kimataifa, kutenga Sh. milioni 500 kwa ajili ya benchi
la ufundi na Sh. bilioni moja kwa ajili ya usajili wa wachezaji kila msimu.
Kutengeneza
brand ya Simba pamoja na vifaa vya klabu kama jezi, kofia, wachezaji kujituma
na kutambua thamani ya klabu ya Simba na kushindana na timu kubwa Afrika.
Mkutano huo
ulihudhuriwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison
Mwakyembe na Waziri wa Utalii Dk. Hamis Kigwangala na Makamu wa Rais wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Michael Wambura.
Awali, klabu hiyo ilisema mwekezaji atamiliki asilimia 50 ya hisa huku
asilimia 10 zikitarajia kugawiwa kwa wanachama waliopo sasa na nyingine 40
kuuzwa kwa wadau wengine.
No comments:
Post a Comment