MWENENDO
mzuri wa Mbao FC umeifanya kampuni ya Hawaii ambao ni wasambazaji wa maziwa ya
Cowbell kumwaga milioni 100 kudhamini klabu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Akizungumza
jana Meneja Masoko wa Hawaii Product Supply Ltd Elisaria Ndeta alisema mwenendo
mzuri wa Mbao umetushawishi kuendelea kuidhamini na msimu huu dau limeongezeka.
“Msimu
uliopita Mbao ndio walituomba udhamini lakini msimu huu sisi ndio tumeomba
kuwadhamini na utaona msimu huu dau limeongezeka kutoka sh. milioni 25 hadi sh
milioni 100,” alisema Ndeta.
Katika
mkataba huo Mbao watakabidhiwa pesa taslimu sh milioni 70 huku sh. milioni 30 zikitolewa kwa njia ya
vifaa.
Kwa upande
wa Mwenyekiti wa Mbao FC, Solly Njashi alisema udhamini huo umekuja wakati
muafaka na utaongeza ari ya kuifunga Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu
unaotarajiwa kuchezwa Jumapili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
“Tunaishukuru
Cowbell kwa kukubali kuendelea kuidhamni Mbao FC na niwaambie tu kuwa udhamini
unaturahisishia maandalizi ya kuifunga Yanga ikiwa ni pamoja na kupandisha
morali ya wachezaji,” alisema Njashi.
Cowbell inaungana na kampuni ya GF Trucks & Equipment kuidhamini
Mbao FC kama wadhamini binafsi wa timu
No comments:
Post a Comment