UNAWEZA
kusema ushindani wa kuwania kiatu cha dhahabu kwa Ligi Kuu Tanzania Bara, umeanza
baada ya mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa kufikisha mabao sita akiwa nyuma ya
mshambuliaji wa Simba Emanuel Okwi kwa
mabao mawili.
Okwi
anaongoza akiwa na mabao nane, katika mechi nane za ligi kuu alizocheza msimu
huu wakati Chirwa amecheza mechi tisa.
Mchezaji wa
Mohamed Rashid wa Tanzania Prisons pia ana mabao sita sawa na Chirwa huku
Ibrahim Ajib wa Yanga akiwa na mabao matano sawa na Ramadhan Kichuya wa Simba
na Habibu Kiyombo wa Mbao FC.
Kwa mtazamo wa
haraka wachezaji wote hawa wanaweza kuibuka mfuungaji bora mwishoni mwa msimu
endapo wataendelea na kasi hii.
Obrey Chirwa
baada ya mchezo dhidi ya Mbeya City juzi alisema kiatu cha dhahabu msimu huu ni
cha kwake.
“Mimi ndio
nitakuwa mfungaji bora kwasababu nilianza ligi vibaya lakini sasa mpira
umetulia mguuni, nitaendelea kufunga kwani ushirikiano na wachezaji wenzangu ni
mzuri,” alisema Chirwa.
Katika
mchezo wa juzi Obrey Chirwa alifunga hat trick ya pili tangu ligi kuu msimu huu
uanze baada ya ile ya Okwi aliyofunga dhidi ya Ruvu Shooting.
No comments:
Post a Comment