KOCHA
Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa amesema hawashindani na Simba bali
wanatimiza malengo waliojiwekea tangu kuanza kwa msimu wa ligi kuu.
Kauli hiyo
aliitoa juzi baada ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa
Uhuru Dar es Salaam dhidi ya Mbeya City na kushinda mabao 5-0 jambo ambalo
wengi wanasema Yanga imeshinda mabao mengi ili kupunguza gepu la mabao dhidi ya
Simba.
“Yanga
haishindani na Simba labda Simba ndio inashindana na sisi kwani tumejiwekea
malengo tangu msimu unaanza na ndio tunayatimiza,” alisema Nsajigwa
Pia Nsajigwa
alisema ushindi huo umetokana na wachezaji kufuata maelekezo ya benchi la
ufundi na kucheza vizuri.
Naye kocha
wa Mbeya City Nsanzurwimo Ramadhani alikiri timu yake kucheza vibaya na kukubali
kubeba lawama zote za kupoteza mchezo huo.
“Timu
haikucheza vizuri na tumepoteza mchezo kwa idadi kubwa ya mabao lakini
wachezaji wasilaume badala yake lawama hizo nazibeba mimi,” alisema Ramadhan
Pia Ramadhan
alisema kuweka kambi sehemu tofauti tofauti haimaanishi kuwa huwezi kufungwa
maana kuna timu zinakwenda kuweka kambi nje ya nchi na zinafungwa.
Huu ulikuwa mchezo wa kwanza kwa Mbeya City kufungwa mabao mengi tangu
ianze kucheza ligi kuu kwani Yanga iliwahi kuifunga mabao 3-0.
Baada ya
kumalizika mzunguko wa kumi Yanga inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 20
nyuma Azam FC yenye pointi 22 sawa na vinara Simba na Mbeya City inashika
nafasi ya tisa ikiwa na pointi na pointi 11.
No comments:
Post a Comment