KOZI ya
Grassroots kwa Vijana kuanzia miaka 6-12, inatarajiwa kufanyika mkoani Mbeya
kuanzia Novemba 27, hadi Desemba Mosi, mwaka huu.
Akizungumza Mkurugenzi
wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi alisema
kozi hiyo itahusisha walimu wa Shule za Msingi za mikoa ya Songwe, Katavi,
Rukwa na wenyeji Mbeya.
“Jumla ya
washiriki 30 watahudhuria kozi hiyo na kila mkoa utatoa washiriki saba
isipokuwa wenyeji Mbeya watatoa washiriki tisa,” alisema Madadi
Kozi hiyo
imezingatia jinsia kwa kila mkoa unatakiwa kutoa idadi sawa au wanawake wawe
wengi zaidi ya wanaume ili kutoa hamasa zaidi kwa wanawake kujifunza.
Kozi hiyo ya
Grassroots itakwenda sambamba na Kampeni ya ‘Live Your Goal’ ikiwa na maana ya
‘Ishi ndoto zako’ itayofanyika Novemba 29, ikiwa na lengo la kutoa hamasa kwa
soka la wanawake.
Kampeni hiyo
ya Live Your Goal inalenga kutoa hamasa kwa wadau waujue, waupende na kuheshimu
soka la wanawake kama ilivyo kwa upande wa wanaume na itachezwa mechi na timu
za wanawake za mkoa wa Mbeya.
Wakati
huohuo, Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Mbeya (MREFA), Elias Mwanjala
amewakaribisha washiriki watakaohudhuria kozi na kusema wapo tayari kupokea
ugeni huo kwa maendeleo ya mpira wa miguu.
Mpango wa
Grass roots kabla ya kwenda kufanyika Mbeya ulifanyika huko Mkoani Lindi.
No comments:
Post a Comment