RAIS
wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amejitosa kwenye
kinyang’anyiro cha uchaguzi mdogo wa Baraza la vyama vya soka Afrika Mashariki
na Kati (Cecafa) unaotarajiwa kufanyika Desemba 2, mwaka huu.
Akizungumza
na gazeti hili kutoka Nairobi jana, Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye
alisema Karia atawania nafasi ya mjumbe wa kamati ya Utendaji katika uchaguzi
huo uliopangwa kufanyika Nairobi siku moja kabla ya kuanza kwa michuano ya
Kombe la Chalenji.
Michuano
ya Chalenji imepangwa kuanza Desemba 3- 17 ambapo timu 10 zinatarajiwa
kushiriki.
“Maandalizi
ya uchaguzi yamekamilika na wagombea wa nafasi hiyo wapo wanane kutoka nchi
wanachama.
Musonye
aliwataja wagombea wengine ni Abdigaani Said wa Somalia, Moses Magogo wa Uganda,
Juneid Basha kutoka Ethiopia, Aimabale Habimana wa Burundi na Rais wa
Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA), Vincent Nzamwita.
Karia
anafuata nyayo za rais wa zamani wa TFF Leodegar Tenga aliyewahi kuwa
Mwenyekiti wa Cecafa.
Kwa
sasa mwenyekiti wa Baraza hilo ni Gaffar Mutasin wa Sudan.
Musonye
alisema uchaguzi wa mwaka huu pia kuna wanawake wawili wanaowania nafasi ya
ujumbe wa kamati ya Utendaji ya Baraza hilo.
Aliwataja
wanawake hao ni Doris Petra wa Kenya na Kourecha Guedi wa Djibouti.
“Tumefurahi
kwamba sasa wigo unapanuka kwenye kamati yetu ya Utendaji tutakuwa na wanawake
ikitokea watachaguliwa,” alisema.
Musonye
alisema, baada ya uchaguzi kutakuwa na mkutano mkuu wa mwaka wa Baraza hilo
ambao utahudhuriwa na wenyeviti na makatibu wakuu wa nchi 12 wanachama.
“Baada
ya mkutano huo, sasa mashindano ya Chalenji yataanza rasmi ambapo tunatarajia
yatakuwa ya kupendeza msimu huu,” alisema.
Michuano
ya Chalenji inafanyika baada ya mwaka jana kutofanyika. Mara ya mwisho
ilifanyika mwaka 2015, Addis Ababa, Ethiopia ambapo Uganda ilitwaa ubingwa.
Baada
ya mkutano huo, mashindano ya kuwania Kombe la Chalenji ambayo mwaka huu
yanashirikisha timu 10 yataanza rasmi kufanyika.
No comments:
Post a Comment