TIMU
ya KMC imepokwa pointi tatu na mabao matatu na kupewa JKT Mlale kwa kosa la kumchezesha
mchezaji Stephano Mwasika katika mechi wa ligi daraja la kwanza uliochezwa
Oktoba 30, 2017 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salam
Akizungumza leo Mtendaji
Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura alisema Mwasika alikuwa na adhabu
ya kadi nyekundu ambayo alitakiwa kukosa michezo mitatu na kulipa faini ya sh.
300,000
“Mwasika
alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumpiga kiwiko mpinzani wake kwenye
mechi dhidi ya Mbeya kwanza iliyochezwa Oktoba 5, 2017 katika Uwanja wa Azam
Complex na alipaswa kukosa michezo mitatu lakini yeye amekosa michezo miwili
tu,” alisema Wambura.
Katika
mchezo huo ambao Mwasika alicheza dhidi ya JKT Mlale uliomalizika kwa sare ya
bao 1-1, KMC ilifikisha pointi 19, hivyo kuondolewa kwa pointi za mchezo huo
inabaki na pointi 18 kileleni mwa kundi B ikifuatiwa na Polisi Tanzania yenye
16 na JKT Mlale, Mbeya Kwanza na Coastal Union ambazo zinawania nafasi ya tatu
zikiwa na pointi 15.
Hii ni mara
pili kwa KMC kupokwa pointi baada ya msimu uliopita kupokwa kwa kosa la kufanya
mabadiliko ya wachezaji wanne badala ya watatu katika mchezo mmoja.
Nayo JKT
Mlale imepigwa faini ya sh. 200,000 kwa kutoingia vyumbani wakati wa mapumziko
katika mechi dhidi ya Coastal Union na Mvuvumwa
imepigwa faini ya sh. 100,000 kwa kosa la kuhudhuria kikao cha maandalizi ya
mechi dhidi ya African Lyon ikiwa na maofisa pungufu.
Coastal
Union imepewa onyo kali kutokana na kuhudhuria kikao cha maandalizi ya mechi ikiwa
na maofisa pungufu na Toto Africans imepewa onyo kali kutokana kuchelewa kikao
cha maandalizi pamoja na waamuzi Jumanne Njige na Bam Bilasho kwa kuchezesha
mechi chini ya kiwango.
Meneja wa
Toto Africans, Yusufu Jumaa amefungiwa miezi miwili na kupigwa faini ya sh.
200,000 wakati mtunza vifaa wa JKT Mlale, Noel Murish na Ofisa Habari wa Toto
Africans, Cuthbert Japhet hadi masuala yao yatakaposilikizwa na Kamati ya
Nidhamu ya TFF.
No comments:
Post a Comment