TANZANIA
imezidi kuporomoka kwenye viwango vya ubora vya Fifa na sasa inashika nafasi ya
142 kutoka nafasi ya 136 iliyokuwa mwezi uliopita.
Kuporomoka
huko kumekuja siku chache baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya
Benin mwanzoni mwa mwezi huu, matokeo ambayo yalitoa matumaini kwa wengi kwamba
huenda ikapanda kwenye viwango hivyo.
Kwa
mujibu wa orodha ya viwango hivyo iliyotolewa kwenye tovuti ya Fifa jana, Benin
iko nafasi ya 82.
Kwa
upande wa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Uganda imeendelea
kuongoza kama ilivyo siku zote ikiwa nafasi ya 74.
Kwa
upande wa Afrika, Senegal ndio inayoongoza ikiwa nafasi ya 23 ikifuatiwa na
Misri nafasi ya 31.
Ujerumani
imeendelea kukaa kileleni katika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Brazil, Ureno,
Argentina, Ubelgiji, Hispania, Poland, Uswisi, Ufaransa na Chile.
No comments:
Post a Comment