Chama cha michezo cha vyuo vikuu Tanzania (Tanzania Universities Sports Asociation “TUSA”) kimeingia makubaliano na Shadaka Sports Management pamoja Clouds Media kwa ajili ya kuendesha mashindano yanayoandaliwa na chama hicho.
Mashindano ya TUSA mwaka huu yanatarajiwa kuanza December 14 hadi 20 mkoani Dodoma kwa kushirikisha vyuo wanachama pamoja vyuo vingine ambavyo vimealikwa.
Mwenekiti wa TUSA Winston Mdegela amesema lengo la mashindano ya vyuo vikuu ni kujenga afya za wanafunzi, kujenga nidhamu na utaifa likini ikiwa ni fursa kwa wachezaji kuonesha vipaji vyao na kutafuta soko.
Mashindano yanayoandaliwa na TUSA yanashirikisha michezo mbalimbali ikiwemo soka, netball, basketball, pooltable, karate, kukimbia na michezo mingine mingi.
“Tunawashukuru wenzetu wa Clouds na Shadaka Sports Management kwa kukubali kuungana nasi katika kuendesha mashundano ya mwaka huu. Tunaomba wadau wa michezo waje kuangalia na kuchukua wachezaji kutoka kwenye mashindano haya kuwapeleka kwenye timu zao”-Mdegela.
Kwa upande wa mwakilishi Shadaka Sports Management na Clouds Media, Issa Masoud amesema wameamua kuingia kwenye mashindano hayo ili kuendelea kuwapa fursa vijana ya kuonesha vipaji vyao.
“Tunaendelea kuishi kauli mbiu yetu ‘tunakugungulia dunia kuwa unachotaka’ tumeingia kushirikiana na TUSA ili kuwafungulia dunia vijana wawe wanavyotaka”-Masoud.
“Ukiachana na kujenga afya, nidhamu na utaifa, michezo ni ajira inayoajiri vijana wengi. Tunataka vijana watoke kupitia sehemu rasmi sio kutoka vichochoroni. Marekani vijana wengi wanaocheza basketball wametoka vyuoni, tunataka ifike mahali wachezaji wetu watoke sehemu zinazotambulika.”
Mwenyekiti wa TUSA Winston Mdegela amewaomba wakuu wa vyuo kuwaruhusu wachezaji kushiriki mashindano hayo kwa sababu kuna faida nyingi watapata.
No comments:
Post a Comment