Akizungumza,
Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alfred Lucas alisema Chirwa ametwaa
tuzo hiyo baada ya kuwashinda Erasto Nyoni wa Simba na Ibrahim Ajibu pia wa Yanga
“Uchambuzi
uliofanywa na Kamati ya Tuzo zinazotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) umetokana na mapendekezo kutoka kwa makocha waliopo viwanja
mbalimbali ambavyo ligi inachezwa msimu huu,” alisema Lucas.
Pia Lucas
alisema Chirwa alitoa mchango mkubwa kwa Yanga mwezi huo ikipata pointi saba
katika michezo mitatu iliyocheza na kupanda katika msimamo wa ligi kutoka
nafasi ya sita iliyokuwepo mwezi Septemba hadi ya pili mwishoni mwa Oktoba.
Yanga iliifunga
Kagera Sugar mabao 2-1 Uwanja wa Kaitaba,Kagera ambapo Chirwa alifunga
bao moja na kutoa pasi ya mwisho ya bao moja na Yanga iliifunga Stand United
mabao 4-0 Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, ambapo Chirwa alifunga bao moja na kutoa
pasi ya mwisho ya bao moja.
Kiwango cha Chirwa
kilionekana pia katika mchezo wa watani wa jadi Yanga na Simba uliochezwa Oktoba
28, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya bao 1-1. Bao la
Yanga lilifungwa na Chirwa, hivyo kwa mwezi huo alifanikiwa kuwa na kiwango cha
juu katika kila mchezo ikiwa ni pamoja na kufunga.
Kwa upande
wa Erasto naye alitoa mchango mkubwa kwa Simba uliowezesha timu hiyo kupata
pointi nane katika michezo minne iliyocheza, akitoa pasi za mwisho za mabao
nne, ambapo Simba ilishinda michezo miwili na kutoka sare miwili, huku Ajibu
akitoa mchango mkubwa kwa Yanga ikiwa ni pamoja na kufunga mabao matatu na
kutoa pasi ya mwisho ya bao moja.
Wachezaji
wengine ambao wameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi msimu huu ni
mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi (Agosti), beki wa Singida United, Shafiq
Batambuze (Septemba).
Chirwa
atazawadiwa Sh milioni moja kwa kuibuka mchezaji bora wa Oktoba kutoka Kampuni
ya Vodacom ambao ndiyo wadhamini wa ligi hiyo
No comments:
Post a Comment