MGOMBEA Zena
Chande wa nafasi ya ujumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Shirikisho la Soka
(TFF) katika uchaguzi wa Chama cha Soka la Wanawake Tanzania (TWFA),
unatarajiwa kutafanyika kesho Dar es
Salaam amesema endapo atachaguliwa tena atahakikisha wanaendeleza soka na
kuboresha.
Zena ambae
ni mhariri msaidizi wa michezo wa gazeti hili alisema kwa kushirikiana na
wenzake wataboresha soka katika kipindi cha miaka minee ambacho watakaa
madarakani.
“Uongozi
wetu tumeanzisha ligi kuu ya wanawake na Taifa cup ya wanawake hivyo tukipewa
ridhaa na wajumbe tutashirikiana kuboresha pale tulipoishia ili ligi kuu iwe na
timu kila mkoa,” alisema Zena.
Mkutano Mkuu
wa TWFA unatarajiwa kufanyika Dar es Salaam na wajumbe kutoka mikoa
mbalimbali waliwasili juzi na jana.
Akizungumza
na gazeti hili, Mwenyekiti Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, Msomi Wakili George
Mushumba, alisema taratibu zote zimekamilika na kinachosubiriwa na wajumbe
kuingia kwenye ukumbi kusikiliza sera za wagombea na kupiga kura.
Tayari Kamati
ya Mushumba ilitangaza majina ya wagombea 11 waliopitishwa kuwania nafasi
mbalimbali katika uchaguzi huo ambao ni Amina
Karuma (Mwenyekiti), Rose Kisiwa (Makamu Mwenyekiti), Somoe Ng’itu (Katibu
Mkuu), Theresia Mung’ong’o (Katibu Msaidizi), Hilda Masanche (Mwekahazina),
Wengine
ni Zena Chande na Salma Wajeso (Mkutano Mkuu wa TFF) Mwamvita Kiyogoma, Triphonia Temba, Jasmine
Soudy na Chichi Mwidege (wajumbe wa kamati ya utendaji)
No comments:
Post a Comment