Kocha mkuu wa Taifa Stars amefanya mabdiliko kadhaa katika kikosi chake kinachotarajiwa kuivaa Lesotho leo usiku katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu wa michuano ya Kombe la Cosafa Castle 2017.
Kipa Aishi Manula, beki Abdi Banda, kiungo Yassin Mzamiru na Elias Maguri walioanza mechi iliyopita dhidi ya Zambia wamewekwa benchi.
Uamuzi huo umewapa nafasi kipa Said Mohamed, beki Nurdin Chona, kiungo Salmin Hoza, na mshambuliaji Stamil Mbonde kuanza mechi kwa mara ya kwanza.
kikosi: Said, Kapombe, Gadiel, Chona, Mbonde – Himid, Hoza, Raphael – Stamil, Msuva, Kichuya
Akiba:Aishi, Kessy, Tamimu, Mzamiru, Ulimwengu, Banda, Maguri
No comments:
Post a Comment