MSANII wa
Bongofleva Ali Kiba ‘King Kiba’ amefurahi mshambuliaji Ibrahim Ajib kusajiliwa
Yanga na kuahidi kumpa ushirikiano japo amekiri kutomfahamu vizuri.
Akizungumza
na gazeti hili, Ali Kiba ambaye ni shabiki wa Yanga alisema kila walipokuwa
wanakwenda uwanjani kutazama mechi za Simba na Yanga watu wanaomfahamu vizuri
Ajib ndio walikua wakimuonesha kwamba yule ndio Ajib.
“Ninasikia
ni mchezaji mzuri na ana kipaji kikubwa, watu wanazungumza, wanampigania, wanalalamika
kwani mchango wake unaonekana ulikuwa mkubwa Simba hivyo amekuja Yanga, namkaribisha
na nitamsapoti,” alisema Ali Kiba
Ajib
alitambulishwa juzi na kusaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Yanga baada
ya mkataba wake na Simba kumalizika
Ajibu mwenye
uwezo wa kufumania nyavu kama mshambuliaji wa kati , mchezeshaji wa juu
anakwenda kukutana na safu tishio ligi kuu kwa ufungaji ya Donald Ngoma, Amisi
Tambwe na Simon Msuva.
No comments:
Post a Comment