KIUNGO mshambuliaji
wa Ndanda FC ya Mtwara, Salum Telela ‘Abo Master’ amesema haumizi kichwa kuhusu
usajili unaoendelea badala yake amejikita katika masomo.
Telela
anayesomea Shahada ya Uhasibu mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Saut tawi la
Mtwara, alisema amepokea ofa nyingi kutoka timu mbalimbali nchini lakini akili
yake ipo zaidi kwenye kitabu kwa sasa.
Kiungo huyo
wa zamani wa Yanga alisema hana uhakika kama ataendelea kuchezea Ndanda msimu
ujao au la kutokana na timu nyingi kuonyesha nia ya kuhitaji saini yake lakini
bado hakuna aliyofikia nayo makubaliano.
“Sifikirii
sana nitakuwa wapi msimu ujao, nimejikita kwenye masomo zaidi japokuwa nimepokea
ofa nyingi kutoka timu mbalimbali ila sio kipaumbele changu ila nitakayokubaliana
nayo maslahi nitajiunga nayo,” alisema Telela.
Timu
mbalimbali zinaendelea kuimarisha vikosi vyao kwa kusajili wachezaji wanaoamini
wataweza kuwasaidia kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi baadae mwezi ujao.
No comments:
Post a Comment