ALIYEKUWA
beki wa kati Mbao FC ya Mwanza Asante Kwasi amesema yuko tayari kutua timu
yoyote ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu ujao
Kauli ya
Kwasi imekuja baada ya kumalizika kwa mkataba wake na Mbao FC ambao nao bado
hawajaonesha nia ya kumwihitaji wala kuzungumza kuhusu mkataba mpya.
Akizungumza
na gazeti hili Kwasi alisema yupo huru baada ya kumaliza mkataba wake na Mbao
mpaka sasa bado hajafanya mazungumzo na timu yoyote.
“Nipo
nyumbani Ghana, mkataba wangu na Mbao umeisha na bado sijafanya mazungumzo na
timu yoyote. Mpira ni kazi yangu ikitokea timu tutakayokubaliana maslahi
nitajiunga nayo haraka,” alisema Kwasi.
Naye
Mwenyekiti wa timu hiyo
Solly Zephania alikiri kutoendelea na beki huyo msimu ujao na kumtakia kila la
kheri katika maisha yake ya soka.
“Msimu ujao
hatutakuwa na Kwasi, mkataba wake umemalizika na tumekubaliana kwa pamoja kuwa
hatutaendelea nae,” alisema Zephania.
Kwasi
alitengeneza kombinesheni nzuri katika safu ya ulinzi imara na nahodha Yusuph
Ndikumana ambayo iliyowasumbua washambuliaji wengi msimu uliopita lakini baada
mkataba kumalizika uongozi ukaamua kumruhusu kutimka.
No comments:
Post a Comment