MSHAMBULIAJI
wa kimataifa raia wa Uganda, Emmanuel Okwi jana usiku aliwasili nchini na
kugeuka bubu.
Okwi ambaye
alipokelewa na Makamu wa Rais wa Simba Gofrey Nyange ‘Kaburu’ katika Uwanja wa
ndege wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam (JNIA) pia walikuwepo wandishi
lakini yeye na Kaburu hawakuongea chochote.
“Nitaitisha
mkutano wa wandishi wa habari mtakuja kuongea naye,” alisema Kaburu.
Alhamisi
iliyopita Mwenyekiti wa Kamati ya usajili wa klabu ya Simba, Zacharia Hanspope
alisema Okwi angewasilia Jumamosi na ndicho kilichotokea.
Okwi
anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili hadi 2019 kuitumikia Simba kwa
ajili ya mashindano mbalimbali kuanzia msimu ujao.
Simba
itashiriki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani baada ya
kutwaa taji la kombe la FA.
Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Uganda “The Cranes”
alijiunga na Simba mwaka 2010 akitokea SC Villa ya Uganda ambako ndiko
alikoanzia soka lake la ushindani.
Okwi aliuzwa Tunisia
na kujiunga na Etoile Du Sahel ambako alijiunga na Yanga mwaka 2014, kabla ya
kurejea tena Simba mwaka 2015 na kuuzwa tena nchini Denmark katika klabu ya
Sonderjsky inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo na mwaka huu anarejea tena
Msimbazi akitokea SC Villa ya nyumbani kwao Uganda ambayo ilimpokea baada ya
kuachana na timu hiyo ya Denmark.
No comments:
Post a Comment