LIGI Kuu ya wanawake ya Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inatarajiwa kuendelea kesho kwa michezo sita kuchezwa
kwenye makundi yote.
Kundi A, linatarajiwa kuna na mchezo
kati ya JKT Queens na Mburahati Queens za Dar es Salaam utakaofanyika kwenye
Uwanja wa Karume, Ilala.
Kadhalika Viva Queens ya Mtwara
itakuwa mwenyeji wa Evergreen ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Nangwanda
Sijaona Mtwara wakati Mlandizi ya mkoani Pwani itakuwa mgeni wa Fair Play
katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Kwa upande Kundi B, Sisterz ya
Kigoma itaikaribisha Baobab ya Dodoma kwenye mchezo utakaochezwa Uwanja wa Lake
Tanganyika Kigoma.
Mchezo mwingine utachezwa Uwanja wa
Samora mkoani Iringa kati ya Panama na Majengo Women ya Singida ilihali
Victoria Queens ya Kagera na Marsh Academy zitapambana kwenye Uwanja wa Kaitaba
Kagera.
No comments:
Post a Comment