KAGERA Sugar leo
inashuka kwenye dimba la Namfua Singida kucheza na Singida United mchezo wa
kombe la Shirikisho.
Akizungumza na gazeti hili kocha wa Kagera
Sugar, Mecky Mexime, alisema mchezo huo ni muhimu kushinda ili wafuze kwenye
hatua ya 16."Kwangu kila mchezo ni fainali, hatudharau timu bali tunaheshimu kwa sababu ni wapinzani wetu, naamini tutashinda japo tupo ugenini," alisema Mexime.
Mchezo mwingine ni kati ya The Mighty Elephant ya Songea na Mashujaa ya Kigoma utakaofanyika Uwanja Majimaji mjini Songea.
Mchezo huo uliahirishwa Jumatano iliyopita, mshindi wake ndiye atacheza na Majimaji katika tarehe mpya itakayotangazwa hapo baadaye kama ilivyo kwa mechi kati ya African Lyon na Mshikamano.
Timu za Simba, Yanga, Azam FC, Toto African na Kiluvya FC zimefuzu hatua ya 16 baada ya kushinda michezo yake.
No comments:
Post a Comment