BEKI wa Kagera
Sugar, Godfrey Taita anapelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu kwa kosa la kuwavamia
waamuzi baada ya mechi na kuwatolea lugha chafu na vitisho kwenye mchezo dhidi
ya Mwadui FC uliochezwa kwenye Uwanja wa Shinyanga.
Akizungumza na
wandishi wa habari jana, Afisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema Taita
alifanya kosa hilo baada ya mchezo kumalizika lakini baadae alidhibitiwa na benchi
la ufundi la timu yake na askari polisi kuingilia kati kumdhibiti.
"Kamati ya nidhamu
itasikiliza shauri la Taita na pia kamati ya Sheria
na Hadhi za Wachezaji ya TFF itasikiliza malalamiko ya Mwadui FC, Polisi Morogoro na Simba kuhusu Hassan Kessy,"
alisema Lucas
Polisi Morogoro inalalamika uhalali
wa usajili wa mchezaji wa Stand United, Kheri Mohamed Khalifa na wachezaji
wawili wa Njombe Mji kucheza mechi bila leseni na sakata la Simba kuhusu Hassan
Kessy.
Pia maombi ya klabu ya Singida
United kuhusu kubadilishiwa mwamuzi kwenye mechi yao yamepelekwa Kamati ya
Waamuzi, wakati maombi ya Alliance Schools, Friends Rangers FC, The Mighty
Elephant na Kariakoo FC yanayohusu uendeshaji yanashughulikiwa na Sekretarieti
ya TPLB.
Kamati ya Sheria na Hadhi za
Wachezaji ya TFF inatarajiwa kukaa wiki ijayo kusikiliza malalamiko dhidi ya
usajili wa wachezaji mbalimbali akiwemo mchezaji Venance Joseph Ludovic na
Hassan Kessy wa Yanga.
No comments:
Post a Comment