KATIBU WA RHINO AFUNGIWA KWA KUDANGANYA KAMATI
Kamati ya usimamizi na uendeshaji imempa adhabu ya Kumfungiwa miezi
mitatu Katibu Mkuu wa Rhino Rangers, Dickson Cyprian Mgalike kwa kosa la
kuidanganya kamati kwa kutoa taarifa potofu katika barua aliyoiandikia
Bodi ya Ligi.
Hapo awali, Kamati ilimuadhibu Mchezaji Sameer Mwinyishere kwa kosa la kumrushia chupa ya maji mwamuzi.
Katibu aliandika barua kusema kwamba Sameer hakufanya kosa hilo na alimtaja mchezaji Yusuf Mputa kwamba ndiye aliyefanya kitendo cha utovu wa nidhamu kwa kumrushia Mwamuzi chupa ya maji.
Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji kwa kushirikiana watendaji wa Bodi ya Ligi ilifanya uchunguzi na kubaini mchezaji Yusuph Mputa hakuwepo kwenye Orodha ya Wachezaji wa siku hiyo. Adhabu hiyo imetolewa kwa kufuata kanuni ya 41(6).
…………………………………………………………………………………………………
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

Post a Comment