Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, April 11, 2013

TANZANIA YAPAA VIWANGO VYA UBORA VINAVYOTOLEWA NA FIFA



USHINDI wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars waliopata katika mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Morocco umesaidia kuipandisha nchi katika viwango vya ubora wa soka duniani.

Katika orodha hizo za kila mwezi zilizotolewa leo Tanzania imekwea kwa nafasi tatu kutoka nafasi ya 119 waliyokuwepo mwezi uliopita mpaka nafasi ya 116 hivyo kuendelea kufanya vyema ukilinganisha na mwaka jana. 

Mabingwa wa Dunia na Ulaya, Hispania wameendelea kung’ang’ania kileleni mwa orodha hizo wakifuatiwa na Ujerumani katika nafasi ya pili na Argentina katika nafasi ya tatu huku kwenye nafasi ya nne kukiwa na ingizo jipya la nchi ya Croatia waliopanda wa nafasi tano mpaka kufikia ya nne na tano bora inafungwa na Ureno.

Kwa upande wa Afrika, Ivory Coast wameendelea kushika nafasi ya kwanza baada ya kupanda kwa nafasi moja duniani mpaka nafasi ya 12 wakifuatiwa na Ghana katika nafasi ya pili ambao wao wamedondoka kwa nafasi mbili mpaka ya 22 duniani. Mali wao wako nafasi ya tatu wakifuatiwa na mabingwa soka barani Afrika Nigeria katika nafasi ya nne na tano bora inafungwa na Algeria.

No comments:

Post a Comment