MWAMUZI aliyechezesha mchezo wa Majimaji dhidi yaYanga Hussein Athuman ameondolewa kwenye orodha ya waamuzi wanaochezesha ligi kwa kosa la kushindwa kumudu mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Majimaji, Ruvuma.
Akizungumza na
wandishi wa habari jana, Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) Alfred
Lucas alisema Athuman alipata alama za chini ambazo
hazimwezeshi kuendelea tena kuchezesha ligi hiyo.
"Mwamuzi Athuman ameondolewa
kwenye orodha na Yanga imetozwa faini ya milioni moja kwa kosa la kutoingia
vyumbani pia kutumia mlango usio rasmi wakati wa kuingia uwanjani,"
Pia mwamuzi Ngole Mwangole amepewa
barua ya onyo kali na kumtaka aongeze umakini wakati akichezesha mechi za Ligi
Kuu baada ya kubainika kukataa bao lililoonekana kutokuwa na mushkeli la Mtibwa
Sugar dhidi ya JKT Ruvu katika mechi iliyofanyika Uwanja wa Mabatini, Mlandizi
mkoani Pwani.
Naye mwamuzi Bryson Msuya amefungiwa
mwaka mmoja kwa kutozingatia sheria ipasavyo wakati akitoa penalti dhidi ya
timu ya Mshikamano FC, na ripoti yake kufanana na ile ya kamishna.
Pia mwamuzi msaidizi, Makongo Katuma
amefutwa katika orodha ya waamuzi kwa kuwapiga vichwa wachezaji wawili wa Mshikamano
FC na mwamuzi wa akiba, Hashim Mgimba ameondolewa kwenye ratiba kwa kuonyesha
muda wa nyongeza tofauti na ule alioelekezwa na Mwamuzi.
Lucas alisema kamishna Fidelis
Ndenga ameondolewa kwenye ratiba ya makamishna kwa taarifa yake kufanana na ya
mwamuzi na kamishna Mnenge Seluja amepewa onyo kwa kosa la kutoripoti kitendo
cha Pamba kuhudhuria kikao cha maandalizi ya mechi ikiwa na wawakilishi watatu
badala ya wanne.
Adhabu zote ni kwa mujibu wa kanuni
za ligi zinazoendesha ligi husika.
No comments:
Post a Comment