BENDI ya Sikinde jana ilifanya kazi ya kurekodi upya wimbo
wa ‘duniani kuna mambo’ na kumshirikisha mwanadada Lady Jay dee.
Wimbo huo wa Sikinde umerekediwa katika studio za FM
zilizopo jijini Dar es Salaam
Katika wimbo huo Lady Jay Dee ameshiriki kuimba kipande la mwanzo kabisa kisemacho "Duniani kuna mambo" kabla ya Bitchuka kuimba pande la pili lisemalo "hata ukifanya jambo Zuri"
Katika wimbo huo Lady Jay Dee ameshiriki kuimba kipande la mwanzo kabisa kisemacho "Duniani kuna mambo" kabla ya Bitchuka kuimba pande la pili lisemalo "hata ukifanya jambo Zuri"
Kwa upande wa kibwagizo kimenogeshwa na Mzee mzima Muhidin
Gurumo na kwa upande wa gitaa la Solo
kasimama Mapesa, Maufi kwenye Rythm na Mbwana Mponda kapiga bass.
Akizungumzia jijini, Msemaji wa Bendi hiyo Jimmy Chika
alisema kuwa wimbo huo utaanza kusikika katika vituo mbalimbali vya radio
kuanzia jumatatu.
“Wimbo huo umeshakamilika na utaanza kusikika kote nchi
nzima kwenye radio na tupo kwenye mkakati wa kurekodi upya nyimbo zingine sita
kwani tunataka kabla ya kumwaga mzee Gurumo hiyo kazi iwe imekamilika”, alisema
Chika
Sikinde ni moja ya bendi kongwe hapa nchini ambazo zimekuwa
zikitunga na kuimba nyimbo zenye kuleta maana kwa jamii.
No comments:
Post a Comment