KILIMANJARO QUEENS YAICHAPA BURUNDI MABAO 3-0
Na Faustine Ruta, Bukoba
Bao zote za Kilimanjaro Queens zilifungwa kipindi cha kwanza, Bao la kwanza limefungwa na Asha Rashid dakika ya 22, Bao la pili lilifungwa na Mwanahamisi Omary dakika ya 30 huku
Bao la tatu lilikuwa la kujifunga wao wenyewe baada ya mabeki wa Burundi kujichanganya na mchezaji Niyonkulu Saidauze kwenye harakati za kutaka kuokoa mpira kwenye eneo hatari dakika ya 33. Hadi dakika 90 zinamalizika Kilimanjaro Queens ndio walikuwa wababe kwa kutoka na ushindi wa bao 3-0. Mchezo huo wa kirafiki wa Kimataifa uliokuwa ni moja ya Timu zote mbili kujiandaa na Michezo ya CECAFA Nchini Uganda. Na Kesho Timu zote mbili zinaelekea jijini Jinja, Nchini Uganda.
Post a Comment