KOCHA wa timu ya Taifa ya Soka, ‘Taifa Stars’ Charles Mkwassa amemrejesha beki wa Yanga, Kelvin Yondani kwenye kikosi kitakachocheza na Nigeria, Septemba 2, kwenye mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika
Akizungumza
na wandishi wa habari, Mkwasa alisema kambi ya hii
ya siku tano itakuwa ya
maandalizi ya Awali na baadae watarejea kwenye timu zao na watakutana
tena Agosti 23, 24 au 25 kwa ajili ya maandalizi ya mwisho.
“Kwenye
kikosi kilichopita Yondani hakuwepo kwa sababu alikuwa anatumikia adhabu ya
kadi mbili za njano na hii ni mechi
muhimu kupata matokeo mazuri ndio maana nimekusanya vijana mapema ili wapate
maandalizi mapema”, alisema Mkwassa,
Pia Mkwassa
alisema kwenye kambi hii wachezaji wa kimataifa hawatakuja bali wataungana na
wenzake Nigeria kwa vile hii mechi haipo kwenye kalenda ya FIFA na kudai
ameweka misingi mizuri kwenye timu na endapo kuna atakuja kocha mwingine
atakuwa na mahali pa kuanzia.
Mkwassa pia amekiri mchezo huu ambao ni wa
kukamilisha ratiba utakuwa mgumu kwani Nigeria wamebadili benchi la ufundi
hivyo kila timu inaungalia mchezo huu kwa jicho la pekee.
Wachezaji
walioitwa ni makipa Deogratius Munishi, Aishi Manula, Benny Kakolanya, mabeki
ni Kelvin Yondani, Agrey Morris, Oscar Joshua Mohamed Husein ‘Tshabalala’, Juma
Abdul na Erasto Nyoni
Viungo ni
Himid Mao, Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya, Jonas Mkude, Ibrahim Jeba, Mwinyi
Kazimoto, Farid Mussa Juma Mahadhi, Hassan Kabunda
Washambuliaji
ni Simon Msuva, Joseph Mahundi, Jamal Mnyate, Ibrahim Ajib John Bocco na
Jeremia Juma
No comments:
Post a Comment