KEPTENI
wa Manchester United, Wayne Rooney, ametwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa
Mwaka kwa 2015 akitetea tena Tuzo ambayo pia aliipata 2014. Hii ni mara ya 4 kwa Rooney kuzoa Tuzo hii ambayo Wachaguaji wake ni Masapota wa Timu ya Taifa ya England. Mapema
Desemba England ilianika Listi ya Wagombea wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa
Mwaka kwa Nchi yao ambapo pia ipo Tuzo kwa Chipukizi Vijana wa chini wa
Miaka 21, U-21. Kepteni wa England, Wayne Rooney, ambae alishinda Tuzo hiyo Mwaka Jana, ni miongoni mwa Wachezaji Watano waliokuwa wakiigombea. Rooney
Mwaka 2015 aliiongoza England kufuzu kuingia Fainali za Mataifa ya
Ulaya, EURO 2016, ambazo zitachezwa huko France Mwezi Juni huku
akihakikisha England inashinda Mechi zao zote 10 za Kundi lao na
kuifungia Jumla ya Bao 5 kwa Mwaka 2015 kwa England huku pia akiivunja
Rekodi ya Sir Bobby Charlton ya Ufungaji Bora katika Historia ya England
kwa kufunga Bao 50 Rekodi ambayo iliwekwa na Charlton Mwaka 1968
alipofunga Bao lake la 49.
GEITA GOLD YAPANDA LIGI KUU
-
Timu ya Geita Gold FC imerejea Ligi Kuu ya NBC baada ya leo kumfunga
Songea United mabao 3-1 wakiwa nyumbani Uwanja wa Nyamkumbu.
Kwa matokeo hayo Geita...
NI SIMBA QUEENS MABINGWA LIGI YA WANAWAKE TZ BARA
-
TIMU ya Simba Queens imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Soka ya
Wanawake Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Mashujaa
Queens jion...
WASIRA AWATOLEA UVIVU WALIOANZA MBIO ZA URAIS
-
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Stephen
Wasira, Leo Machi 27, 2026, Mjini Bunda Mkoa wa Mara alipokuwa akiweka
jiwe la ms...
Post a Comment